Header Ads Widget

MMILIKI WA KAMPUNI YA KUFUA UMEME YA IPTL, HARBINDER SETH AHUKUMIWA KULIPA FIDIA YA SH BILIONI 26

Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth, kulipa fidia ya Sh 26bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatano Juni 16, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ya Uhujumu uchumi namba 27/2017 ilipoitwa mahakamani hapo kwa makubaliano.

Seth ameachiwa leo baada ya kulipa milioni 200 ambapo pesa zilizobaki atalipa kwa awamu kulingana na makubaliano baina yake na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ambapo atatakiwa kulipa kwa kipindi cha miezi 12 (mwaka mmoja).
Chanzo: Mwananchi na Millardayo.com

Post a Comment

0 Comments