Header Ads Widget

ALLY MAYAY, OSCAR NA JIMMY KINDOKI WAKATWA URAIS TFF, WAPINZANI WA KARIA WABAKI WAWILI


Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Benjamin Karume, leo Juni 16, 2021 imewatangaza waliokosa vigezo vya kuendelea na mchakato wa uchaguzi kwa nafasi ya Urais kuwa ni Oscar Oscar, Ally Mayay Tembele na Ally Saleh.

Waliopita kuwania Urais wa TFF ni Evans G. Mgeusa, Wallace Karia na Hawa Mninga.

WALIOKATWA KUGOMBEA URAIS WA TFF
Kamati ya Uchaguzi wa TFF kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Benjamin Karume amewatangaza waliokosa vigezo vya kuendelea na mchakato wa uchaguzi kwa nafasi ya Urais.

ALLY MAYAY TEMBELE ❌
- Hakuthibisha Vyeti vyake kwa Kamishna wa Viapo
- Hakukamilisha idadi ya wadhamini [Endorsement]

ALLY SALEH ❌
-Hakuthibisha Vyeti vyake kwa Kamishna wa Viapo
- Hakuwa na wadhamini [Endorsement]

OSCAR OSCAR ❌
- Hakuwa na wadhamini [Endorsement]


Post a Comment

0 Comments