Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Kambarage mjini Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa soko hilo ambao ulishindwa kufanyika kutokana na madai kuwa watendaji wa serikali wameingiza majina ambayo hayakuwepo awali, hivyo kulazimika kufanyika uchaguzi wa mpito
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAFANYABIASHARA katika Soko la Kambarage lililopo Manispaa ya Shinyanga mkoani hapa wamelazimika kufanya uchaguzi wa mpito wa viongozi wa soko hilo baada ya kushindwa kufanya uchaguzi mkuu kwa kile walichoeleza kuwa baadhi ya watendaji wa serikali wamebadilisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali na kuweka majina mengine.
Wakizungumza na wakati wa mkutano wa uchaguzi huo, baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo, walisema kuwa uchaguzi huo hauwezi kufanyika kutokana na baadhi ya viongozi wa serikali kuuingilia na kuuvurga kwa kuingiza masuala ya siasa badala ya kuangalia maslahi mapana ya wafanyabiashara hao.
Mwandishi wa habari hii alifika eneo la mkutano huo na kushuhudia mgogoro huo ambao umedumu kwa masaa kadhaa na kusababisha uchaguzi viongozi wa soko hilo kushindwa kufanyika, huku viongozi walio hudumu kwa kipindi cha miaka 5 wakijiudhuru na kuacha nafasi zao hali iliyo pelekea baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi huo kuchagua uongozi wa mpito.
Wakizungumzia sakata hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage, Malick Juma na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kambarage, Selemani Katonja ambao ni wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo, wamewataka wafanyabiashara kuwa wavumilivu na kuheshimu uongozi wa mpito ulio chaguliwa ili kuepusha athari ukiwemo ugomvi na vurugu zinazoweza
kupelekea uvunjifu wa amani katika soko hilo na kusababisha baadhi yao kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mmoja wa wafanyabiashara hao akitoa malalamiko mbele ya mwenyekiti wa mtaa na kaimu mtendaji wa kata ya Kambarage wakati wa mkutano huo
Mmoja wa waliokuwa viongozi wa soko la Kambarage akitangaza kujiuzuru nafasi ya makamu mwenyekiti
Viongozi wa mpito wa soko hilo waliopitishwa baada ya uchaguzi mkuu kushindwa kufanyika
0 Comments