Header Ads Widget

WAKULIMA SHINYANGA WATAKIWA KUGEUKIA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Mhandisi wa kilimo na umwagiliaji mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Christopha Mashalla akizungumza na mwandishi wetu leo ofisi kwake

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
ILI kuhakikisha wakulima mkoani Shinyanyanga wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini wakulima wametakiwa kubadili fikra na kuanza kulima kilimo cha umwagiliaji mkoani humo.

Wito huo umetolewa leo May 20, 2021 na Mhandisi wa kilimo na umwagiliaji mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Christopha Mashalla wakati akizungumza na Shinyanga Press Club Blog ofisini kwake, ambapo ameeleza kuwa zaidi ya Sh. Bilioni 4 zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa sikimu ya umwagiliaji katika kata ya Nyida halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ukarabati wa mradi wa sikimu ya umwagiliaji Mwamalili katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.

Mashalla ameeleza kuwa baada ya kuanzisha ofisi ya kilimo na
umwagiliaji mkoa wa Shinyanga wameweka mkakati madhubuti wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa wa kulima kilimo cha umwagiliaji pamoja na kuainisha maeneo maalum watakayojenga sikimu za umwagiliaji katika mkoa wa Shinyanga.

Aidha Mhandisi Mashalla amesema kuwa iwapo watapata fedha hizo wataweza kujenga na kukarabati miradi hiyo hali itakayo wapa fursa wananchi wengi kuchangamkia.
Mhandisi Christopha Mashalla akizungumza na mwandishi wetu leo ofisi kwake


Post a Comment

0 Comments