Header Ads Widget

MWENYEKITI WA KITONGOJI USHETU ASAKWA TUHUMA ZA MAUAJI KWENYE KILABU CHA POMBE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba

Na Damian Masyenene, SHINYANGA 
JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamsaka Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikindika Kata ya Ushetu Wilaya ya Kipolisi Ushetu mkoani hapa, Andrew Adam kwa tuhuma za mauaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba, tukio hilo lilitokea Aprili 18 saa 4 usiku katika Kitongoji cha Ikindika, Kijiji cha Kidana, Kata ya Ushetu,Tarafa ya Dakama, Wilaya ya kipolisi Ushetu Mkoa wa Shinyanga, ambapo mtuhumiwa alimuua Daud Lubambula (49) kwa kumpiga chupa kichwani na kwenye mkono wa kulia.

Baada ya kipigo hicho, Daud alivuja damu nyingi na kupoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha afya Ushetu.

Kamanda Magiligimba ametaja chanzo cha tukio hilo kuwa ni ugomvi uliotokana na ulevi kati ya marehemu na mtuhumiwa wakiwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.

Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.


Post a Comment

0 Comments