Header Ads Widget

BASHIRU, POLEPOLE 'OUT' CCM, SHAKA, CHONGOLO WASHIKA NAFASI ZAO

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dk. Bashiru Ally

Na Shinyanga Press Club Blog
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya viongozi wake wakuu kitaifa ikiwemo nafasi ya Katibu Mkuu iliyokuwa inashikiliwa na Dk. Bashiru Ally pamoja na nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi iliyokuwa inashikiliwa na Hamphrey Polepole.

Katika Mabadiliko hayo, CCM imempitisha Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu Mpya wa chama hicho, huku nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ikichukuliwa na Shaka Hamdu Shaka.

Mabadiliko hayo yamefanyika leo na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao Maalum kilichoketi leo mara tu baada ya Mkutano Mkuu wa chama hicho chini ya Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM na kuridhia mapendekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti kujaza nafasi kadhaa na kufanya mabadiliko katika Sekretariati kuu ya CCM.

Dk. Bashiru anatolewa kwenye nafasi hiyo ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu alipoondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi Machi 31, mwaka huu na kuteuliwa kuwa mbunge.

Kwa sasa, Dk. Bashiru Ally na Hamphrey Polepole ni wabunge wa kuteuliwa na Rais wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ambapo, Dk. Bashiru Ally aliteuliwa na Rais wa awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan wakati akitangaza baraza lake jipya la Mawaziri Machi 31, Mwaka huu, huku Humprey Polepole akiteuliwa kuwa mbunge na Rais wa awamu ya tano, Hayati Dk. John Magufuli.

Safu mpya ya Sekretarieti ya CCM

Katibu Mkuu wa CCM- Ndg Daniel Chongolo (Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni)

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM- Ndg Shaka Hamdu Shaka

Katibu wa Uchumi na Fedha Frank George Hawasi aendelee na nafasi yake

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ngebela Lubinga aendelee na nafasi yake

Katibu wa NEC Oganaizesheni -Ndg Mama Maurdin Kastiko

( Ndg Pereira Silima atapangiwa majukumu mengine ya kitaifa)

Naibu Katibu Mkuu Bara- Christina Mndeme (Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma)(Ndg Rodrick Mpogolo atapangiwa majukumu mengine ya kitaifa)

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar- Abdallah Juma Sadala Mabodi anaendelea na nafasi yake.

Post a Comment

0 Comments