Header Ads Widget

RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO MCHAKATO WA CHATO KUWA MKOARais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza mchakato wa kuifanya wilaya ya Chato kuwa mkoa, ambao tayari umeshaanza, uendelee na serikali itajiridhisha kama vigezo vyote vinavyotakiwa vimetimia.

“Nina taarifa mchakato wa Chato kuwa mkoa umeanza, niwaagize kumaliza mchakato huo katika ngazi zenu mtuletee serikalini tutaangalia vigezo, kama vimekidhi hatuna budi kufanya hivyo, kama vigezo havikukidhi tutaelekeza mfanye nini ili vigezo vikidhi.

“Ninachotaka kuwaambia Watanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameitwa na Mungu na ameitika, leo tunakwenda kumsitiri. Tunachokwenda kukisitiri ni kiwiliwili chake, lakini maono, mikakati na falsafa ya Hapa ni Kazi itaendelea kuwepo na tutaendelea kuifanyia kazi.

“Tunakwenda kumpumzisha Baba, Shujaa,Jemedari wetu, ameitwa na Mungu na ameitika leo tunakwenda kukisitiri kiwiliwili chake tu lakini maono na mikakati yake ya Hapa Kazi tu tutayaendeleza, tusiyumbe, tudumishe Upendo, tuendeleze Taifa.

“Kwa ndugu zetu wa Chato najua kwamba ule wasiwasi ulioelezwa hapa uko mioyoni mwenu, nataka niwahakikishie kinachofuata ni kutekeleza kwa ahadi zote zilizoko ndani ya ilani ya CCM na zile alizozitoa yeye mwenyewew kwa watu wake,” Rais Samia Suluhu.

Post a Comment

0 Comments