
Meneja wa Kanda ya Magharibi kutoka benki ya NMB,  Sospeter Magese akizungumza na baadhi ya wananchi kwenye uzinduzi wa kampeni maalumu iliyofanyika katika stendi kuu ya mabasi wilayani Kahama iliyokwenda kwa jina la 'Bonge la mpango' itakayoendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu
Na Neema Sawaka, Kahama
WANANCHI   wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga  wametakiwa kuhifadhi fedha zao kwenye taasisi za kifedha ili waweze kujipatia faida itakayowawezesha kujinyanyua kiuchumi  kutokana na mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakianzishwa.
Hayo yalisemwa leo   na Meneja wa Kanda  ya Magharibi  kutoka benki ya NMB,  Sospeter Magese kwenye  uzinduzi wa  kampeni   maalumu iliyofanyika  kwenye stendi kuu ya mabasi  wilayani Kahama iliyokwenda kwa jina la 'Bonge la mpango' itakayoendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu.
Magese amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kutumia taasisi za fedha kuhifadhi fedha zao eneo ambalo ni salama  kwa kuweza  na  kujiongezea kipato  kupitia  mashindano yanayoanzishwa  yenye tija.
“Kampeni  hii itakuwa ni kanda ya magharibi inayojumuisha mikoa minne   ambayo ni  Tabora,Simiyu,Kigoma na Shinyanga     na imelenga kuhamasisha wateja na wasio wateja kufungua akaunti   nakujishindia  gari,  pikipiki  ya mizigo yenye  miguu mitatu  na fedha taslimu,” amesema Magese.
Magese ameeleza kuwa katika kampeni hiyo maalum yenye lengo la  kurejesha faida kwa wateja  nakuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa wananchi   ambapo imeanza  rasmi jana na   kiasi cha Sh. millioni  550  kimetengwa  kuendesha zoezi hilo kipindi cha miezi mitatu.
Aidha Magese  alisema kuwa  zawadi zitatolewa kila wiki kwa washindi  pia katika kipindi hiki cha mavuno  Benki  ya NMB imetoa elimu kwa wananchi kuhakikisha  wanahifadhi  fedha

 Meneja NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magese (aliyeshika bendera)  akiwa na wafanyakazi wa benki hiyo Kanda ya Magharibi na tawi la Kahama wakizindua kampeni ya Bonge la Mpango katika Stendi ku ya Mabasi Kahama Mkoani Shinyanga

Meneja NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magese  akionyesha moja ya zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu itakayotolewa kwa washindi katika kampeni ya Bonge la Mpango


Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi na tawi la Kahama wakifanya uhamasishaji katika kampeni iliyozinduliwa ya Bonge la Mpango, leo katika stendi kuu ya mabasi mjini Kahama.