Header Ads Widget

KIKWETE: WALIOSEMA SIKUMTAKA JPM NI WAGANGA NJAA

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) na Rais wa awamu ya tano, hayati Dk. John Magufuli (Picha na: Mtandao)


Rais mstaafu, Jakaya Kikwete amesema alimuamini zaidi rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli na ndio maana alimteua kuwa waziri katika wizara tatu tofauti katika kipindi cha miaka 10 ya utawala wake akisema, “alikuwa jembe langu.”

“Waswahili wanasema akutukane hakuchagulii tusi unaposikia minong’ono kwamba unasikia Kikwete hakumtaka Magufuli mimi labda Kikwete mwingine nimewasimulia leo mchakato tulivyokwenda na yale majina matano nilikuja nayo mimi tumepambana nayo mpaka yakatoka na la kwanza lilibaki kuwa la JPM nililoliweka mie nashukuru kwenda hadi mkutano mkuu ikawa hivyo hivyo.”

“Oooh... Kikwete anamchukia Magufuli eeh labda mwingine si mimi namchukiaje mtu uliyemkabidhi ilani ya uchaguzi na ameitekeleza kwa kiwango cha juu sana lakini nikasema dunia waganga njaa wengi wanapata ulaji wao kwa kuongopa,” amesema Rais mstaafu Jakaya Kikwete katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Magufuli.

Post a Comment

0 Comments