Header Ads Widget

BUNGE LAMPITISHA KWA KISHINDO DK. MPANGO

Dkt. Philip Mpango

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha kwa asilimia 100 jina la aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya jina lake kupendekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai, Dkt. Mpango amepigiwa kura halali 363 ambazo ndio jumla ya wabunge waliokuwepo kwenye Mkutano wa tatu wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Machi 30, 2021 wakati zoezi la kura likifanyika.

Uteuzi huo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati. Dk. John Pombe Magufuli na aliyekuwa Makamu wake Mhe. Samia Suluhu Hassan kuapishwa kushika nafasi ya Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kufanya nafasi ya Makamu wa Rais iwe wazi na leo kujazwa rasmi.

Post a Comment

0 Comments