Header Ads Widget

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAIDHAMINI SIMBA SC

Muonekano wa Jezi za timu ya Simba SC utakavyokuwa kwenye mechi zake za makundi ya Klabu Bingwa Afrika (Picha na Simba SC).

Na Damian Masyenene
KLABU ya Simba SC ya Dar es Salaam imeingia makubaliano na Wizara ya Maliasili na Utalii ya kutumia neno 'VISIT TANZANIA' kwenye jezi za timu hiyo katika mechi zake za kimataifa hususan za Makundi ya Klabu Bingwa Afrika zinazotegemewa kuanza wiki ijayo.

Simba imeingia makubaliano hayo leo jijini Dodoma katika mkutano wao na waandishi wa habari, ambapo inaelezwa kuwa hatua hiyo ni kutokana na sheria za Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ambalo haliruhusu timu kuwa na udhamini wa kampuni za kubashiri kwenye michuano yake kuanzia ngazi ya makundi kutokana na CAF kuwa na mdhamini kampuni ya kubashiri ya 1XBET.

Baada ya kuingia makubaliano hayo, Klabu ya Simba imeandika kwenye ukurasa wao wa Instagram maneno haya "Mabingwa wa nchi SIMBA SC tumeingia makubaliano na Wizara ya Maliasili na Utalii ya kutumia neno VISIT TANZANIA kwenye jezi ambazo tutazitumia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. #VisisTanzania #NguvuMoja,"

Simba inadhaminiwa na kampuni ya kubeti ya SportPesa, ambayo nembo yake itaendelea kuonekana kwenye jezi ya Simba katika mashindano mengine yakiwemo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (FA).

Tazama picha mbalimbali za makubaliano hayo
Mtendaji Mkuu wa Simba (CEO), Barbara Gonzalez akisaini mkataba wa makubaliano hayo


Post a Comment

0 Comments