Header Ads Widget

'WANAWAKE LAKI MOJA' YAZINDULIWA RASMI, KUWASOMESHA WATOTO WA MAMA ALIYEUAWA KWA MTWANGIO


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kushoto) akimlisha Keki Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga, Anaskolastika Ndagiwe katika hafla ya uzinduzi wa asasi hiyo leo mjini Shinyanga.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
ASASI ya Kiraia ya Wanawake Laki Moja ambayo inajishughulisha na kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto pamoja na kupambana na umaskini imezinduliwa rasmi leo mkoani Shinyanga.

Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wanawake wa kada mbalimbali mkoani hapa na mikoa jirani kutoka asasi za kiraia, Serikali, vyama vya siasa na taasisi za kifedha, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.

Akizindua asasi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, amewapongeza katika kuendeleza mapambano ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto na kuinuana kiuchumi kwani imekuja katika muda muafaka ambao mkoa huo unapambana na kutokomeza matukio hayo.

Ambapo, RC Telack amewataka wanawake hao kutoa taarifa za matukio ambayo wanafanyiwa wao na watoto wao ili wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria na kumaliza vitendo hivyo vya ukatili ndani ya jamii.

Telack amesema baadhi ya wanawake wamekuwa hawatoi taarifa za matukio ya ukatili kwakuwa wahusika wa vitendo hivyo ni ndugu zao wa karibu au waume zao, huku wakihofia kuvunja mahusiano, na kusababisha wahusika kutochukuliwa hatua, na vitendo hivyo vya ukatili kuendelea kuwapo na hatimaye kuleta madhara baadae ikiwamo kupoteza uhai na ndoa za utotoni.

Aidha amewaonya wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwalaza watoto chumba kimoja na wageni, bali wakalale nao, na chumba hicho wamuachie mgeni, sababu wageni wengine ndio wamekuwa wahusika wakuu wa kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili kwa kuwachezea michezo michafu.

"Wanawake jiungeni kwenye vikundi vya ujasiriamali ili mpate asilimia 10 fedha za mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya mitaji na kuendesha biashara mbalimbali na kujikwamua kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi kwa waume," amesisitiza.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Katibu wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoa wa Shinyanga, Pendo Sawa, amesema lengo la asasi hiyo ni kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake, pamoja na kujenge ana uwezo wa kuinuana kiuchumi.

Anasema Asasi hiyo ilianzishwa mwaka jana, na sasa imezinduliwa rasmi leo kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto vikiwamo vipigo, ubakaji, kulawiti, kutekeleza familia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

“Changamoto ambayo tumeiona Asasi ya Wanawake Laki Moja juu ya kuendelea kwa matukio ya ukatili mkoani Shinyanga dhidi ya wanawake na watoto, ni tatizo la mila na desturi kandamizi, ambazo zimekuwa mwiba kwa jinsi ya kike na kuendelea kunyanyasika ndani ya jamii,”anasema Sawa.

“Kutokana na changamoto hii ya kuendelea kwa matukio ya ukatili mkoani Shinyanga, tunaomba Serikali ishirikiane na asasi za kiraia kutoa elimu kwa wananchi namna ya kupambana na matukio ya ukatili ndani ya jamii, ikiwamo na kuzijua sheria ya kupigania haki zao hasa kwa wanawake wajane ambao wamekuwa wakidhurumiwa mali wanapofiwa na waume zao,”ameongeza.

Naye Mwenyekiti wa Wanawake Laki Moja Mkoa wa Shinyanga, Annaskolastika Ndagiwe, ameeleza kusikitishwa na matukio ya ukatili ambayo yanaendelea kutendeka mkoani Shinyanga, huku wahusika wa matukio hayo wakishindwa kuchukuliwa hatua stahiki, na kuendelea kuishi Uraiani kitendo ambacho amebainisha kinaumiza sana.

Amesema kuna baadhi ya matukio ameshayatolewa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya tukio la watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili, lakini cha ajabu wahusika wa matukio hayo hakuna hatua zozote za kisheria ambazo zimechukuliwa juu yao, jambo ambalo linawapa ugumu katika kuendeleza mapambano ya kupinga ukatili ndani ya jamii.

Pia katika uzinduzi huo wa wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga, wameguswa na tukio la Mwanamke ambaye aliuawa na mume wake kwa kupigwa ngumi na Mtwangio, ambaye aliacha watoto watatu, ambapo Mkurugenzi wa Shule ya Little Treasure Ruth Mwita, ameahidi kuwasomesha watoto wawili kwenye shuleni yake, ambapo mmoja atasomeshwa na Asasi hiyo ya wanawake Laki Moja.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akizungumza kwenye uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga.
Katibu wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Taifa Josephine Ngonda, akizungumza kwenye uzinduzi wa Asasi hiyo Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga Anaskolastika Ndagiwe, akizungumza kwenye uzinduzi wa Asasi hiyo.
Analyse Kaika, kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga kwa Niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Debora Magiligimba.
Katibu wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga Pendo Sawa, akisoma taarifa ya Asasi hiyo.
Meneja Biashara kutoka Benki ya CRDB Mwanahamisi Iddi, akielezea fursa za wanawake zilizopo kwenye Benki hiyo.
Meneja Biashara kutoka Benki ya NMB Fred Limbu, akielezea fursa zilizopo kwenye Benki hiyo.
Wanawake wakiwa kwenye uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga ukiendelea.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack Kushoto, akikata Keki kuzindua Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani humo.
Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga Anaskolastika Ndagiwe.kulia, akimlisha Keki Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, mara baada ya kumaliza kuzindua Asasi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, kushoto akimlisha keki Katibu wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Pendo Sawa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, kushoto akimlisha Keki, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga Catherine Langau, kwenye uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Zoezi la ulishaji Keki likiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wapili Kushoto, akimkabidhi Cheti cha Pongezi Katibu wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Taifa Josephine Ngonda.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wapili kushoto, akitoa cheti cha Pongezi kwa Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga Anaskolastika Ndagiwe.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wapili kushoto, akitoa cheti cha Pongezi kwa Benki ya CRDB.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, kushoto, akitoa cheti cha Pongezi kwa Kampuni ya Lulekia.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akiwa amebeba Zawadi kutoka kwa Asasi ya Wanawake Laki Moja kutokana na Mchango wake mkubwa wa kupambana kutokomeza matukio ya ukatili wa Jinsia.
Katibu wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Taifa Josephine Ngoda, kulia, akimkabidhi Taulo la Kike, Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola kwa ajili ya wanafunzi ambao ni wahanga wa mimba na ndoa za utotoni ambao wanalelewa na Shirika hilo.
Viongozi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga na Taifa, wakitoa mchango wa msaada kwa mtoto ambaye mama yake aliuawa na Baba yake kwa kipigo, ambapo pia mtoto huyo atasomeshwa kwenye shule binafsi ya Little Treasure.
Mkurugenzi wa Shule Binafsi ya Little Treasure Ruth Mwita, akielezea kuguswa na watoto ambao mama yao aliuawa na mumewake kwa kupigwa na Mtwangio, na kuahidi kuwasomesha bure watoto wawili wa mwanamke huyo shuleni kwake.
Awali wanawake wakiwa kwenye maandamano wakielekea kwenye uzinduzi wa Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea na jumbe mbalimbali kwenye mabango za kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia.
Maandamano yakiendelea na jumbe mbalimbali kwenye mabango za kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Wanawake kutoka Asasi ya Wanawake Laki Moja Mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja kwenye Ofisi ya dawati la Jinsia la Polisi Mkoani Shinyanga.

Picha zote na Marco Maduhu

Post a Comment

0 Comments