Header Ads Widget

POLISI MBEYA WATUHUMIWA KUMUUA KIJANA WA MIAKA 17, RPC AJIBU

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei

Kijana Ivan Kabambala, mwenye umri wa miaka (17) mkazi wa Kagera, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, baada ya kupigwa risasi mgongoni na polisi mkoani humo.

Akizungumzia tukio hilo, Baba mzazi wa marehemu, Aggrey Kabambala, amesema kuwa tukio limetokea majira ya saa 2:00 usiku katika eneo ambalo marehemu alikuwa anafanyakazi ya kuosha magari.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya, William Ntinika, ametoa pole kwa familia ya marehemu Ivan na kuwaomba wananchi wa Mtaa wa Kagera kuwa watulivu wakati wakisubiri ukweli wa tukio hilo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema marehemu Ivan ni miongoni mwa vijana 20 waliokuwa wakipanga njama za kufanya uhalifu na kwamba baada ya kupata taarifa Jeshi la Polisi ilifika eneo la tukio.




Post a Comment

0 Comments