Header Ads Widget

HOFU YA TALAKA NA KUACHIKA YAWA KIKWAZO WANAWAKE KUSHIRIKI KWENYE VYOMBO VYA MAAMUZI ZANZIBAR

Yumna Mmanga akiwasilisha mada ya umuhi wa jamii uwaunga mkono wanawake katika nafasi mbali mbali za uongozi katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni mkoa wa kaskazini Unguja.

Na Muhammed Khamis,TAMWA-Z’bar
Imelezwa kuwa tatizo la wanawake wengi kutoshiriki katika vyombo mbali mbali vya maamuzi pamoja na kushika nafasi za uongozi baadhi yao huogopa kupewa talaka na kuachika kwenye ndoa zao.

Hayo yamelezwa huko Mkokotoni mkoa wa kaskazini Unguja wakati wa mkutano maalumu ulioandaliwa na TAMWA-Z’bar na kuwashirikisha baadhi ya wawakilishi wa vyama vya siasa na viongozi wa shehia wenye lengo la kuhamaisha jamii kuwaunga mkono wanawake katika kushiriki kwenye uongozi.

Akiwasilisha mada katika mkutano huo, Yumna Mmanga amesema Zanzibar imejaliwa kuwa na neema kubwa ya wanawake wenye uwezo mkubwa na wengine ni wasomi lakini cha kushangaza hadi leo hii wamebaki kuwa mama wa nyumbani jambo ambalo anaamini kuna sababu ikiwemo ya kuhofia kupewa talaka.

Alisema kitendo cha wanawake wengi kuhofia kupewa talaka bado ni miongoni mwa vikwazo vinavyowakwamisha wanawake wengi na ipo haja jamii kubadilika ili kutoa fursa kwa wanawake.

Alieleza kuwa hwenda hofu hio kwa wanaume inatokana na baadhi ya wanaume uelewa mdogo wakiamini kuwa mwanamke kushiriki kwneye ugozi hwenda wakadharau waume zao jambo ambalo halina msingi.

Thuwayba Juma Hussein aliewahi kugombea nafasi ya Uakilishi jimbo la Mahonda kupitia chama cha ACT Wazaledo alisema alipoamua kugombea alikutana na changamoto mbali mbali.

Alisema cha kushangaza zaidi ni watu waliokua karibu yake walimvunja moyo na kumshangaa alipofanya maamuzi hayo lakini hakurudi nyumba ingawa wengine walimtaka ajitoe.

Alisema kutokana na kujiamini kwake aligombea na wanaume watatu kwenye hatua ya awali ya kutafuta uteuzi wa Chama na kwamba alifanikiwa kuwa mshindi wa mwanzo na chama chake pia kumrudisha kuwa mgombea.

Kwa upande wake Ali Sleiman ambae ni katibu wa sheha ya mkokotoni alisema katika shehia yake kuna wanawake ambao wamepewa nafasi kuwa kwenye kamati za shehia na wanafanya kazi zao vizuri sana.

Alisema kwa uwajibikaji wa wajumbe hao ambao ni wanawake kwenye kamati hio ni wazi kwamba wanawake wengi wakipewa nafasi kumbe wana uwezo mkubwa kiutendaji.

‘’Sikua nikifahamu awali kama wanawake wana uwezo kiasi kile kwenye kazi niliamini wanawake ni watu wasikua na uwezo kabisa awa’’aliongezea.

Katibu wa Baraza la vijana wilaya ya kaskazini A Unguja,  Fatma Sharif Ibrahim alisema awali katika shehia ya kipange wakati anateuliwa sheha mwanamke jamii ilimdharau sana na kuelewa wazi wazi kuwa hataweza kuongoza shehia hio.

Alisema licha ya kusemwa kwake vibaya lakini mwanamke huyo hakukata tamaa na alifanya kazi zake kwa weledi mkubwa na hadi sasa amekua kivutio kwa walio wengi.

Wakati hayo yakijiri imelezwa kuwa changamoto nyengine ni mifumo ya vyama vya siasa kupitia katiba zao bado hakujawekwa fursa sawa za kikatiba ambazo zingeweza kuwabeba wanawake.

Alisema kwenye vyama vyote vya sasa Tanzania bado katiba zao hazijaweka wazi kutoa fursa za upendeleo kwa wanawake wanatakaoshindana na wanaume kwenye kura za awali.

‘’Kutokana na kukosekana kwa kipengele cha katiba wanawake wengi wanaposhindana na wanaume katikam kura za awali watashindwa na hawana mwega wakuegemea kutokana na kukosekana kipengele muhimu cha katiba’’aliongezea.

Aidha alitolea mfano katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2020 wanawake wengi walijitokeza kuomba ridhaa za vyama vyangu jambo ambalo alisema ni wazi kuwa wanawake wengi wamehamasika.

Silima Juma Abdalla kutoka kaskazini Unguja anasema wanawake wengi Zanzibar bado wanakabiliwa na hofu wanapotaka kugombea na kueleza kuwa hwend ahofu hile ikawa inawakwanza na kukosa kujiamini hata hao wanafanikiwa kugombea.
Silima Juma Abdalla mwakilishi wa Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa kaskazini Unguja akichangia kuhusu umuhimu wa wnajamii kuwaunga mkono wanawake katika nafasi za uongozi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku moja wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada katika ukumbi wa chuo cha Amali mkokotoni mkoa wa kaskazini Unguja.


TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807