Header Ads Widget

TAIFA STARS YAONJA USHINDI CHAN, YAICHAPA NAMIBIA 1-0 SASA MATUMAINI KIBAO

Wachezaji wa Taifa Stars wakipongezana baada ya kupata bao la kuongoza dhidi ya Namibia kwenye michuano ya CHAN nchini Cameroon (Picha na Azam Sports 2)

Na Damian Masyenene
BAADA ya kuanza vibaya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) yanayoendelea nchini Cameroon, hatimaye leo Timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' imeonja ladha ya ushindi baada ya kuibuka kidedea kwa kuichapa Namibia bao 1-0.

Stars ambayo ipo kundi B katika michuano hiyo, imepata ushindi huo kupitia bao pekee la dakika ya 65 lililofungwa na Winga Farid Mussa.

Ushindi huo unafufua matumaini ya Tanzania katika michuano hiyo, ambapo sasa inakamata nafasi ya tatu katika kundi lake ikiwa na alama tatu ikiwa nyuma ya vinara Guinea wenye alama nne sawa na Zambia, ambapo katika mchezo ujao Stars itakutana na vinara Guinea.

Tanzania ilianza vibaya michuano hiyo ikipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa majirani zao, Zambia. hivyo mchezo ujao dhidi ya Guinea ambao ni wa mwisho kwa Tanzania katika kundi hilo utakuwa wa kufa na kupona ili kuhakikisha wanakata tiketi ya kusonga mbele.


TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807