Header Ads Widget

SIMBA YAFUNGA MWAKA KIBABE, YAITUNGUA IHEFU FC 4-0MABINGWA watetezi wa ligi kuu bara Simba, leo Desemba 30 wameufunga mwaka 2020 kibabe, baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wake dhidi ya Ihefu Fc kwa Magoli 4-0 na kuvuna alama tatu muhimu kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mnyama Simba ameingia kwenye mchezo huu akiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 5-0 ilioupata dhidi ya Majimaji kwenye dimba hilo jumapili ya Desemba 27.


Magoli ya Simba yalifungwa beki Mohamed Hussein dakika ya 10’ na magoli mawili yakifungwa na mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 16’ na 40’ na mshambuliaji aliyeingia kipindi cha pili Chris Mugalu dakika ya 84 alihitimisha karamu hiyo ya magoli.

Baada ya ushindi wa leo wekundu wa msimbazi wamefikisha alama 35, baada kucheza michezo 15, timu ya Yanga ambayo kesho Desemba 31 inashuka dimbani kuwakabili Tanzania Prisons inaoongoza msimamo wa ligi kwa alama 43 baada ya michezo 17.

Post a Comment

0 Comments