Header Ads Widget

MKURUGENZI MWANGULUMBI AWAFUNDA WASICHANA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Wasichana 30 wakiwa kwenye ufungaji wa mafunzo yao, wakisiliza nasaha za mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi.

Na Marco Maduhu, Shinyanga 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi, amewataka wasichana katika manispaa hiyo ambao hawakuendelea na masomo na wapo mitaani, wasijiingize kwenye makundi mabaya ikiwamo kufanya biashara ya kuuza miili yao (ngono), bali wajiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ili wapate mikopo na kujikwamua kiuchumi. 

Mwangulumbi alibainisha hayo wakati akifunga mafunzo kwa vijana 30 wa kike, ambao walikuwa wakipewa elimu ya makuzi, haki, afya ya uzazi, na ujasiriamali, kwa ajili ya kuwaepusha na visababishi vya kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) pamoja na kupata mimba zisizo na matarajio ambayo yaliandaliwa na Shirika la Restless Development na kufadhiliwa na UNFPA. 

Alisema katika Mkoa wa Shinyanga kuna fursa nyingi za kufanya biashara, lakini vijana wengi wamekuwa wakifikili ili kuwa na maisha mazuri lazima uajiriwe, na kubainisha matajiri waliowengi hapa nchini ni wafanyabiashara, na kuwataka wasichana ambao wapo mitaani wasikate tamaa, bali wachangamkie fursa zilizopo ili wajikwamue kiuchumi na kuendesha maisha yao. 

“Wasichana ambao mpo mitaani acheni kusubili kuwezeshwa, bali safari ya maisha yenu ina anza na wewe mwenyewe, mjiamini, mjitambue, na kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali, pesa zipo Halmashauri za kuwawezesha, ila mje na mawazo mazuri ya kibiashara hasa ya kufungua viwanda vidogo,” alisema Mwangulumbi. 

“Vijana mnatakiwa mbadilike na kuacha kulia lia maisha magumu, maisha siyo mpaka uajiriwe, tumieni fursa zilizopo kwenye maeneo yenu kufanya biashara, na kazi ya Serikali ni kujenga mazingira wezeshi ya kisera na miundombinu bora ya kufanya biashara,”aliongeza. 

Adha alisema ndani ya miaka mitano tangu (2015-2020), Halmashuari hiyo imeshatoa fedha za mikopo kwa vikundi vya ujasiriamali Shilingi Bilioni moja, kwa ajili ya kuwainua kiuchumi. 

Naye Mwenyekiti wa kikundi hicho cha wasichana, Miriam Mgaya, awali akisoma taarifa, alisema mabinti wengi ambao wapo mitaani walioshindwa kuendelea na masomo, wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi za kimaisha, na kusababisha kuingia kwenye makundi ya kufanya biashara ya ngono ili wapate mahitaji. 

Alisema wasichana wakipewa elimu ya afya ya uzazi na kuwezeshwa kwenye vikundi vya ujasiriamali na kupata mikopo ya Halmashauri, itawasaidia kwa kiasi kikubwa kujikomboa kimaisha, na kuacha kujiingiza kwenye makundi mabaya ambayo huaribu ndoto zao kwa kupata ujauzito ama virusi vya ukimwi. 

Kwa upande wake mratibu wa miradi kutoka Shirika la Restless Development Mkoani Shinyanga John Eddy, ambao wanatekeleza mradi wa vijana tunaweza, alisema lengo kuu la mradi huo ni kupunguza visababishi vya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana, na ndio maana wanatoa elimu ya kujitambua na jinsi ya kukidhi mahitaji yao. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya wasichana 30 kutoka Kata tatu za manispaa hiyo ambazo ni Oldshinyanga , Ndala, na Ndembezi.
Afisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka Shirika la Restless Development, Costantine Shayo, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo.
Mratibu wa miradi kutoka Shirika la Restless Development Mkoani Shinyanga John Eddy, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Wasichana 30 wakiwa kwenye ufungaji wa mafunzo yao, wakisiliza nasaha za mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi.
Wasichana 30 wakiwa kwenye ufungaji wa mafunzo yao, wakisiliza nasaha za mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi.
Ufungaji mafunzo ukiendelea.
Ufungaji mafunzo ukiendelea.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kambarage Malick Mmbasha, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mwabundu Kata ya Ndala Colleta Kitungulu, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo.
Picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo.


Post a Comment

0 Comments