Header Ads Widget

MADIWANI KISHAPU WAAPISHWA, MTIHANI WA KWANZA KWAO NI UJENZI WA SHULE NA VYUMBA VYA MADARASA

Sehemu ya madiwani 40 kutoka kata mbalimbali za halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambao walishinda kwenye uchaguzi mkuu wa Oktob a 28, 2020, wakila kiapo cha kuwa madiwani rasmi leo wilayani Kishapu.

Na Marco Maduhu, Kishapu 
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, wameapishwa rasmi na kupewa jukumu la ujenzi wa shule, vyumba vya madarasa na madawati, ili kukabiliana na changamoto ya wanafunzi kusoma kwenye miti na kukaa chini. 

Zoezi la kuapishwa madiwani hao limefanyika leo Desemba 14, 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, lililosimamiwa na Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Kishapu Amana Ismail. 

Akizungumza wakati wa kufungua zoezi la kuapisha madiwani hao, Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese,  amesema jukumu la kwanza ambalo wanatakiwa kwenda kuanza nalo ni kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati, ili wanafunzi watakao anza masomo januari mwakani wasisome kwenye mazingira ambayo siyo rafiki. 

"Madiwani mmeshakula kiapo leo na kuwa madiwani Rasmi, hivyo nawaomba jukumu la kwanza ambalo mnatakiwa kwenda kulifanya ni kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati, ili wanafunzi wasikae chini na kusomea kwenye miti," amesema Kengese. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akitoa salamu kwenye zoezi hilo la kuwaapisha madiwani hao, amesema wilayani yake mwaka ujao inategemea kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza na wale wa darasa la saba, hivyo kuna baadhi ya Kata zinatakiwa kujengwa shule mpya. 

Amezitaja Kata hizo kuwa ni Lagana, Sekebugolo, Isoso, Mwaweja, Shagihilu, Mwasubi, na Bupigi, na kuwataka madiwani hao wakafanye kazi hiyo ya ujenzi wa shule mpya pamoja na ujenzi huo wa madarasa na madawati, kwa kushirikiana na wananchi kuchangia shughuli hizo za maendeleo. 

Nao baadhi ya madiwani hao akiwamo Edward Nkuba kutoka Kiloleli, wamesema watakwenda kulifanyia kazi suala hilo la upungufu wa vyumba vya madarasa, madawati, na ujenzi wa shule, kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na Mgodi wa Almas Williamson Diamond. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Emmanuel Jonsoni, amewaomba madiwani kuwa na ushirikiano wa kutosha kwenye ujenzi wa miundombinu hiyo ya shule, ambapo tayari walikuwa wamesha anza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya shule. 

Akitoa neno kwa madiwani hao, Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniphace Butondo (CCM), ameahidi ushirikiano na madiwani hao, ambapo januari mwakani ataanza ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu hiyo ya shule, na kuona namna ya kutatua changamoto zake ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati. 

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba akizungumza kwenye zoezi la uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese, akizungumza kwenye uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Jonsoni, akizungumza kwenye zoezi hilo la Uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu William Jijimya, akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la kula kiapo na kupigiwa kura za ndio kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Underson Mandia, akizumgunza mara baada ya kumaliza kula kiapo na kupigiwa kura za ndio kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Kishapu Amana Ismail, akiwaapisha Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mara baada ya kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakila kiapo cha kuwa madiwani Rasmi, mara baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakila kiapo cha kuwa madiwani Rasmi, mara baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.Post a Comment

0 Comments