Header Ads Widget

HERI JAMES AMJULIA HALI MWENYEKITI MSTAAFU UVCCM TAIFA, ANDREW MASANJE MJINI KAHAMA

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Heri James akimsikiliza Mwenyekiti Mtaafu wa (UVCCM) Taifa Comrade Andrew John Masanje Nyumbani kwake kahama jana

Salvatory Ntandu, Kahama 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Heri James amemtembelea Mwenyekiti Mtaafu wa (UVCCM) Taifa Comrade Andrew John Masanje wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga katika ziara yake ya kikazi ya siku mmoja kwa lengo la kumjulia hali yake ya afya baada ya kupata taarifa kuwa hali yake sio nzuri. 

Akiwa nyumbani kwa Mzee Masanje leo, Comrade James amesema kuwa UVCCM Taifa inatambua mchango wake katika ujenzi wa Umoja huo na wataendelea kuwa pamoja nae hadi afya yake itakapoimarika,na kuwataka Viongozi wa Umoja huo Kahama kuendelea kumsaidia pindi anapopata matatizo mbalimbali. 

"UVCCM Taifa inatambua kazi zilizotekelezwa na Mzee Masanje wakati wa Uongozi wake sisi Vijana tunajifunza kwake kwani uwepo wake kwetu sisi ni hazina,tutaendelea kumtunza ili tuendelee kujifunza mambo mazuri kutoka kwake kwa ustawi wa Umoja wetu’’ amesema James. 

Ameongeza kwa kusema kuwa UVCCM imemletea msaada kidogo ili uweze kumsaidia ambayo ni pamoja na mchele kilo 30 sukari kilo 20,Maharage kilo 20 mafuta lita 10 pamoja na fedha Taslimu zaidi ya Shilingi milioni mmoja ili ziweze kumsaidia katika kipindi hiki ambacho afya yake ilidhoofika kutokana kusumbuliwa na Maradhi. 

Akizungumza baada ya kupokea ugeni wa Comrade James Mzee Masanje alimshukuru sana kwa Kumkumbuka na kukubali kuja kumtembelea nyumbani kwake Kahama pamoja na kumletea msaada wa vyakula na fedha kwaajili ya kujikimu. 

"Nimefarijika sana kumwona Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Heri James kuja na ugeni wake kunitembelea nyumbani kwangu,sina cha kuwapa ila Mwenyezi Mungu atawalipa kwa kila kile mlichotoa,Sisi wazee waastaafu tutaendelea kuwaombea Sala ili muendelee kutimiza majukumu yenu vizuri ya kukitumikia chama chetu cha Mapinduzi,’’ameeleza Masanje. 

Amesisitiza kuwa kwa sasa afya yake inaendelea kuimarika kila siku kuwaomba watanzania kuendelea kumwombea ili apone haraka na kuwaomba vijana kuendelea kufanya kazi kwa Uzalendo,weledi na uaminifu ili kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kushika hatamu katika uongozi wa Tanzania. 

Comrade Andrew Masanje ndio Mwenyekiti wa Kwanza wa UVCCM Taifa 1977 hadi 1982 na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kitaifa katika serikali na Chama ambapo amewahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama 2007-12. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Heri James akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha kabla ya kuambatana nae kwenda kumtembelea Mwenyekiti Mtaafu wa Wa kwanza (UVCCM) Taifa Comrade Andrew John Masanje mjini Kahama.
Comrade Masanje akibadilishana mawazo na wageni waliofika nyumbani kwake kumjulia hali wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Heri James
Comrade Masanje akibadilishana mawazo na wageni wake
Heri James akifurahia jambo na Comrade Masanje alipomtembelea nyumbani kwake mjini Kahama kumjulia hali
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Heri James akisalimiana Mwenyekiti Mtaafu wa (UVCCM) Taifa Comrade Andrew John Masanje Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga katika Ziara yake ya Kikazi ya Siku mmoja 
 
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807