Header Ads Widget

ASKOFU SANGU AENDESHA IBADA MKESHA WA KRISMAS AKISISITIZA KUDUMISHA AMANI, DC MBONEKO ATUMA SALAMU KWA WANANCHI


Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Liberatus Sangu  akiingia kanisani kwa ajili ya kuendesha Ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya Kristmas.

Na Marco Maduhu, Shinyanga 
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Liberatus Sangu, amewataka Watanzania kudumisha amani ya nchi. ili waishi kwa upendo, utulivu, na kufanya shughuli za maendeleo. 
Askofu Sangu amebainisha hayo jana wakati akiendesha Ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya Kristmasi, iliyofanyika usiku kwenye Kanisa kuu la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo na kuhudhuliwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko. 

Alisema watanzania wanapaswa kuilinda amani ya nchi, ambayo iliasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuacha kuichezea ili kutoingia kwenye machafuko. 

“Nawaomba watanzania tuidumishe amani ya nchi yetu, bila amani hakuna upendo, furaha, wala maendeleo, na kuna mataifa yana wivu sana na Tanzania, na kutaka tufarakane ili kuvuruga amani tuliyonayo, tusikubali bali tuilinde na kuidumisha amani ambayo tuliachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,” alisema Sangu. 

Katika hatua nyingine Askofu Sangu aliipongeza Serikali mkoani Shinyanga, kwa kupunguza tatizo la mauaji ya vikongwe, na kuomba kasi iongezwe zaidi ya kumaliza kabisa mauaji hayo ya watu wasio na hatia, hasa katika maeneo ya vijijini ambapo bado yanaendelea. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, alimwahidi Askofu Sangu kuwa maombi yake yote ambayo ameyaomba kwa Serikali yatatekelezwa, huku akiwataka wananchi wawe na hofu ya Mungu na kutenda yaliyo mema na kuacha kutenda maovu, pamoja na kusheherekea sikukuu kwa amani na utulivu. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Askofu Liberatus Sangu akiendesha ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya Kristmas katika kanisa kuu la Ngokolo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akitoa salam za Serikali kwenye mkesha wa siku kuu ya Kristmas.

Waumini wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa siku kuu ya Kristmasi
Waumini wakiendelea na ibada kwenye mkesha wa siku kuu ya Kristmas.
Ibada ikiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wakwanza kushoto, akiwa na waumini wakiendelea kusali kwenye ibada ya mkesha wa siku kuu ya Kristmas.
Ibada ikiendelea.

Ibada ikiendelea.
Waumini wakitoa sadaka.
Waumini wakiendelea kutoa Sadaka.

Awali Askofu Sangu, akibariki waumini wakati akiingia Kanisa kuendesha Ibada ya mkesha wa siku kuu ya Kristmas.


Askofu Sangu akibariki waumini kwenye ibada ya mkesha wa siku kuu ya Kristmas.
Awali Askofu Sangu, akiingia kanisani kuendesha Ibada ya siku kuu ya Kristmas.
Awali Askofu Sangu, akiingia kanisani kuendesha Ibada ya siku kuu ya Kristmas.

Post a Comment

0 Comments