Header Ads Widget

JPM AMTUMBUA MKURUGENZI WA IGUNGA TUHUMA ZA KUTWAA ARDHI YA WANANCHI

Revocatus Kuuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Revocatus Kuuli.

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kuuli leo Desemba 28, 2020 kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kutwaa ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na matumizi mabaya ya fedha za maduhuli ya Serikali.

JPM amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Phillemon Sengati kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja.


Post a Comment

0 Comments