Header Ads Widget

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUWASIKILIZA NA KUWAPA NAFASI WATOTO KUONESHA VIPAWA


Watoto wa Kanisa la IEAGT Kambi ya Waebrania Shinyanga ambao wameadhimisha wiki yao kanisani hapo kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo mahubiri, maigizo, mistari ya kwenye Biblia takatifu na burudani za nyimbo za injili.

Na Shinyanga Press Club Blog
KANISA la International Evangelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT) la Mjini Shinyanga leo Novemba 8, 2020 limeadhimisha wiki ya watoto kanisani hapo, huku wazazi na walezi wakiombwa kuwapa nafasi watoto waweze kuonesha vipawa vyao, kuwasaidia kukua kiroho na kimwili na kuwajengea mazingira ya kujieleza na kuwaondolea hofu pamoja na kukua kitaaluma.

Maadhimisho hayo yamefanyika kanisani hapo katika Misa ya Jumapili,ambapo watoto hao walipata fursa ya kutoa huduma kanisani, kucheza nyimbo za kumsifu Mungu, kuonyesha umahiri katika kukariri mistari ya Biblia takatifu, kuhubiri neno, kufanya maigizo mbalimbali na burudani ya nyimbo.

Akitoa neno kwa niaba ya watoto, Nazareth David amesema ni vyema wazazi wakajenga ukaribu na watoto wao ili waweze kuwasikiliza na kujua changamoto wanazozipata shuleni, nyumbani na mtaani na kufahamu namna ya kuwasaidia na kuwapa ushauri.

Nazareth ameongeza kwa kueleza kuwa suala la malezi halipaswi kuwaachia walimu peke yao, bali wazazi wawafuatilie shuleni kujua maendeleo yao na makuzi, kuwapa moyo na kuwahamasisha wafanye vizuri kimasomo na kushiriki neno la Mungu.

Akihubiri neno, mtoto Grolia Paul amezungumzia juu ya waumini kutoruhusu huzuni kutawala maisha yao na kuzaa hasira na chuki, ikiwemo wazazi kutochukua hatua mbaya pale watoto wao wanapofanya vibaya kwenye masomo na mambo mengine kwa kuwakatisha tamaa.

"Ni vyema tukatumia hekima kwenye hasira, maneno, usaliti, kuangukaa katika maisha na wakati wa magonjwa,kwa sababu ukiruhusu huzuni izae hekima basi utaletewa haki, kufunguliwa milango ya baraka, kujiokoa na mauti na kuwa na nguvu mpya," amesema.

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa hilo, Mchungaji David Mabushi amewahimiza wazazi kushiriki vyema katika malezi kiroho na kimwili kwa kuwatia moyo watoto wao na pia watoto kuungwa mkono pale wanapoamua kushiriki katika kazi za Mungu.

"Wazazi tuwe karibu na watoto wetu ili tujue vipawa na uwezo wao, tuwatie moyo na tuwaandae kuwa taifa na wazazi wa kesho....lakini pia nawakumbusha waumini mhudhurie mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika Novemba 12 hadi 15, mwaka huu katika uwanja wa Kambarage hapa Shinyanga," amesema.
 
Askofu wa Kanisa hilo, David Mabushi akizungumza na waumini wake juu ya malezi ya watoto na umuhimu wa kuwasikiliza na kuwapa nafasi ya kuonyesha vipawa vyao
 
 Nazareth David akitoa neno kwa niaba ya watoto
 
Mtoto Gloria Paul akihubiri neno la Mungu kanisani hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Watoto ndani ya kanisa hilo
 
Mzee wa Kanisa, Rehema Suleman akiongoza maombi ya kumaliza ibada kanisani hapo
 
Mlezi wa watoto Kanisani hapo, James John

Mwalimu wa watoto hao, Tryphina Joshua
 
Watoto wakitoa huduma ya kuimba

Watoto wakitoa burudani ya kucheza

Watoto wakitumbuiza kwa nyimbo

Watoto wakionyesha umahiri wa kukariri mistari ya kwenye Biblia Takatifu


Mtoto Evance Henry (aliyeshika kipaza sauti) akionyesha umahiri wa kukariri vifungu vya kwenye Biblia Takatifu


Mojawapo ya maigizo yaliyofanywa na watoto hao kuonyesha namna wanadamu wanapochelewa kupata watoto wanakata tamaa

Mabango yakionyesha matatizo mbalimbali yanayowakumba wanadamu

Mtoto akiigiza namna hofu inavyowatesa wanadamu
Watoto wakiigiza namna Bwana Yesu Kristo alivyokuwa akizungumza na wanafunzi wake


Burudani ya nyimbo za kumsifu Yesu Kristu zikiendelea

Burudani zikiendelea


Waumini wakiendelea kufuatilia kwa umakini huduma na burudani zinazotolewa na watoto

Waumini wakiwafuatilia watoto wanavyomtukuza Mwenyezi Mungu

Kiongozi wa watoto hao, Nazareth David akiwaongoza kuimba wimbo kwa ishara

Watoto wakiingia kanisani hapo kwa ajili ya kutoa sadaka kwenye kuadhimisha wiki ya watoto ndani ya kanisa hilo
Watoto wakijongea kuwasilisha sadaka yao kwa Askofu wa kanisa hilo, David Mabushi

 Askofu Mabushi akiwashukuru watoto hao baada ya kupokea sadaka waliyoiwasilisha
Waumini wa kanisa hilo wakiomba na kushukuru wakati wa ibada ya Jumapili
Maombi yakiendelea

Waumini wakiendelea kuombaWaumini wakisikiliza mahubiri kanisani hapo
Post a Comment

0 Comments