Header Ads Widget

WACHIMBAJI WADOGO 8 WAJERUHIWA BUHEMBA MARA

Moja ya eneo la mgodi wa Buhemba

Wachimbaji wadogo nane wajeruhiwa kwa silaha za jadi ikiwamo mapanga, visu pamoja na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao katika machimbo ya dhabu ya Irasanilo, Buhemba yaliyopo wilayani Butiama mkoani Mara chanzo kikiwa ni kugombania maduara ya uchimbaji.

Wakizungumza baadhi ya majeruhi hao wamesema wakiwa wanaendelea na uchimbaji ndani ya shimo, walivamiwa na kundi la watu ambao walianza kuwashambulia na nondo mawe pamoja na kuwachoma na visu sehemu mbalimbali za mwili.

Akizungumzia tukio hilo mmiliki na katubu wa duara hilo namba tisa A, ambalo limevamiwa, Mwajuma Seif amesema kabla ya tukio hilo duara hilo lilikuwa na mgogoro huku uongozi wa wachimbaji hao wadogo mkoani Mara, wakatoa tamko la kulaani tukio hilo la kikatili kwa wenzao.

East Africa Television, ilimtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi na alizungumza kwa njia ya simu na kukiri kuwepo kwa tukio hilo na hapa anaeleza zaidi.

Post a Comment

0 Comments