Header Ads Widget

WAAMUZI YANGA NA SIMBA KESHO WATAJWA

Mwamuzi Elly Sasii(Pichani) ndiye atakayeamua mchezo kati ya Yanga na Simba utakaochezwa kesho.

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF limetaja majina ya waamuzi watakaochezesha dabi kati ya Yanga na Simba itakayochezwa kesho katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika orodha hiyo mwamuzi wa kati ni Elly Sasii akisaidiwa na Mohamed Mkono na Frank Komba ambao ni washika vibendera(Line1&Line 2).

Abdallah Mwinyimkuu na Aboubakar Mturo ni waamuzi watakaokaa nyuma ya magoli ya timu zote mbili huku Ramadhani Kayoko akiwa ni mwamuzi wa mezani.

Kamishna wa mchezo ni Philip Olando wakati mtathmini wa waamuzi ni Pascal Shinganga.

Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa kesho majira ya saa 11 kamili jioni huku Yanga ndio wenyeji wa mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments