Header Ads Widget

DPP AWAONYA WAUZAJI WANAOFICHA VIFAA VYA UJENZI ASEMA KUFANYA HIVYO NI UHUJUMU UCHUMI

  .        Mkurugenzi  wa Mashtaka Nchini Bw.Biswalo Mganga akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi nchini kuacha kuficha Vifaa hivyo.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Biswalo Mganga amewaonya wauzaji wa vifaa vya Ujenzi kufuatia baadhi yao  kuficha Sementi na Mabati kwa lengo la  kuongeza bei  ili kujipatia faida kubwa zaidi, na  kusema kuwa kufanya hivyo  ni  kosa la Jinai

Bw. Mganga ameeleza kuwa watu  wote wanaofanya hivyo wanafanya kosa la uhujumu uchumi ambalo limeanishwa katika Sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 jela   pamoja na  kutaifishwa  mali kwa yeyote atakayekamatwa kwa kutenda kosa hilo.

Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo Jijini Dodoma leo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika yaliyokuwa na lengo la kufahamu mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya  Mashtaka tangu kuanzishwa kwake ambapo ameeleza kuwa imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake.

Aidha, amesema kuwa jukumu la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni kuhakikisha kuwa Haki, Amani na Usalama vinapatikana nchini kwa Maendeleo ya Taifa.                                                                                      Mwonekano wa nembo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma
                                           Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Biswalo Mganga akusoma Dira ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
       Mwonekano wa mbele wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) lililoko Jijini Dodoma

Share: 

Post a Comment

0 Comments