Header Ads Widget

DK ABBAS AKAGUA ENEO LA UJENZI WA UWANJA WA KISASA WA SOKA DODOMA, UJENZI KUANZA KARIBUNI

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas (wa mbele kulia) akikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa soka jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Jumamosi, Novemba 14, 2020, ametembelea na kukagua eneo ambalo Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Uwanja Wa Kisasa wa Michezo jijini Dodoma.

Dkt. Abbasi amesema eneo hilo lenye ukubwa wa eka zaidi ya 320 ni kubwa mara 10 zaidi ya eneo vilipo viwanja mbalimbali vya Taifa jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa kwa ukubwa huo eneo hilo linaweza pia kutumika kuweka vituo vingine vya shughuli za burudani ikiwemo ujenzi wa ukumbi mkubwa wa michezo ya ndani na sanaa za maonesho (indoor art and sports arena). 

Katibu huyo Mkuu ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, amesisitiza ahadi iliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uwanja mkubwa Dodoma itatekelezwa haraka iwezekanavyo.Picha kwa hisani ya Dk. Hassan Abbas

Post a Comment

0 Comments