Header Ads Widget

WADAU WA MICHEZO MSALALA WAOMBA KUJENGEWA UWANJA ILI KUKUZA VIPAJI VYA VIJANA

 


Mkuu wa Wilaya akizungumza na baadhi ya wachezaji wa timu ya watumishi FC  inayomikiwa na Halmasahuri ya msalala baada ya mchezo wa mshindi wa tatu kumaliza na timu hiyo kushinda mabao 11-0 dhidi ya timu ya bulyanhulu.


Na Neema Sawaka,Kahama

WADAU wa mchezo soka Katika Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameiomba Halmashauri hiyo kuwasaidia wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu katika shule za sekondari kwa kupitia Michezo kwa kujenga uwanja katika wa mpira wa miguu ili kuweza kuhimili katika kuwatafutia  karo za shule.

 

Mratibu wa mashindano ya kombe la Mahona,Patrick Mahona alisema wamesaidia Wanafunzi wengi waliopo katika mazingira magumu kusoma kupitia  mchezo wa mpira wa miguu kila mwaka ambapo mpaka sasa wamewasomesha  wanafunzi 15 kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.


Aliyasema hayo  wakati wa fainali za mashindano hayo juzi  ambayo hufanyika kila mwaka katika Halmashauri ya Msalala, huku lengo kubwa likiwa ni kusaidia watoto kuwalipia karo za shule pamoja na mahitaji mengine waliopo katika mazingira magumu.


Mahona ambaye ni Mtendaji wa Kata katika kata ya segese amesema  kwa sasa mashindano hayo yanachezwa katika uwanja wa shule ya msingi Segese na iwapo halmashauri itawajenga uwanja wake hata idadi ya wanafunzi inaweza kuongezeka.

 

Mahona amesema mashinado hayo kwa sasa yanatimiza miaka saba tangu yaanzishwe  mwaka 2014 yakifadhiliwa na baadhi ya wadau katika kata ya segese yakiwemo makampuni ya madini ya wachimbaji wadogowadogo ya Mmilic Gold plant namba nne, Masangi Gold Plant, Domain Gold  pamoja ba Azan Logistc ikiwa lengo kuu ni kuinua vipaji katika kata hiyo.

 

Alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo ya ukosefu wa uwanja Uongozi wa ligi hiyo kwa kushirikiana na kijiji husika umetafuta eneo ambalo litafaa kujengwa uwanja wa mpira na kuiomba Halmashauri ya Msalala iwasaidie  fedha za kulipia eneo hilo.

 

Alisema kuwa Halmashauri ya Msalala haina eneo la uwanja wa michezo ambapo wameomba kata ya segese iwe kituo cha michezo mbalimbali  katika Halmashauri hiyo ya msalala.

 

Mahona alisema kuwa katika mashinado hayo yalijumuisha timu 16 huku zikiwa katika makundi manne  ambapo katika mchezo wa jana wa kutafuta mshindi wa kwanza mpaka wa tatu  timu ya watumishi kutoka Halmashauri ya Msalala ilikuwa mshindi wa tatu bada ya kuifunga Bulyanhulu mabao 11-0.


 Mshindi wa pili alikuwa ni Young Boys ya Segese ambayo ilipata kichapo cha mabao 7-2 dhidi ya Mguu Target,Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ilikuwa timu ya Mguu Target.

 

Mshindi wa kwanza ilipata Kombe na seti ya jezi na kiasi shilingi milioni moja wakati wa pili Young Boys ilipata sh 400,000pamoja na jezi huku timu ya watumishi ikipata sh 200,000.

 

Akifunga mashindao hayo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha aliwataka wadau mbalimbali wa michezo katika jamii kujitokeza kwa wingi katika kuinua vipaji na kuongeza kuwa kama vitaendelezwa vipaji vinaweza  kujipatia ajira  na kufika mbali.

 

Mashindao ya Kombe la Mahona ambayo hufanyika kila mwaka  yamejijengea sifa kwa kutoa baadhi ya wachezaji akiwemo Adam Salamba ambaye yuko Namungo FC, Mnyonge Athumani aliyopo JKT, Revocatus Malima aliyepo Gwambina FC, Samson Mdeleke Mbeya City pamoja na  Moris Mahela Gwambina FC.

 


Post a Comment

0 Comments