Header Ads Widget

NEC YAHIMIZA USHIRIKIANO KUHAMASISHA WAPIGA KURA MIL.29 WAJITOKEZE OKTOBA 28

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Oktoba 2,2020 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna katika Manispaa ya Shinyanga.

Na Damian Masyenene, Shinyanga
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeendelea kukutana na wadau na makundi mbalimbali katika jamii kwa kutoa elimu na kujenga ushirikiano utakaosaidia kuwaelimisha wapiga kura kujitokeza kwa wingi kushiriki katika michakato ya uchaguzi hasa siku ya kupiga kura ili kuleta ufanisi wa zoezi la uchaguzi huo.

Ambapo, leo Oktoba 2, 2020 Tume hiyo imekutana na makundi ya waandishi wa habari, wazee, wenye ulemavu, wanawake, vijana, watendaji wa serikali, Asasi za kiraia na viongozi wa dini katika mkoa wa Shinyanga kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Shinyanga, ukihudhuriwa pia na Mratibu wa Uchaguzi mkoani hapa, Fabian Kamoga na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi.

Akifungua semina hiyo, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Baraka Leonard ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za sheria wa tume hiyo, amesema wanaendelea kusisitiza kampeni za kistaarabu zisizo hamasisha uvunjifu wa amani, ambapo amewaomba wadau hao kuwaelimisha wananchi, wagombea na wafuasi wao kutotumia matamshi ya kuvunja sheria za nchi kwa kisingizio cha uchaguzi.

Leonard ameeleza kuwa tume hiyo itaendesha uchaguzi huo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kuufanya uwe huru na wa haki kwa kuweka mazingira sawa ya ushindani, huku akibainisha kuwa siku ya kupiga kura Oktoba 28, 2020 wapiga kura wote wenye mahitaji maalum wakiwemo wajawazito, wazee na wenye ulemavu mbalimbali watapewa kipaumbele.

"Tume inatarajia mtapeleka ujumbe sahihi kwa wafuasi (wananchi) wenu ili uchaguzi wetu ufanikiwe, muendelee kuviasa vyama na wagombea wazingatie maadili na waepuke vitendo vya uvunjifu wa amani," amesema.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Nuru Riwa amebainisha kuwa jumla ya wapiga kura 29,188,347 waliandikishwa, ambapo wapiga kura 29,059,507 wapo Tanzania Bara na 128,840 Zanzibar, huku pia jumla ya wapiga kura 566,352 waliandikishwa na ZEC.

Pia amesema kuwa kati ya wapiga kura hao 29,188,347 walioandikishwa, wanawake ni 14,691,743 sawa na asilimia 50.33, wanaume ni 14,496,604 ambao ni sawa na asilimia 49.67, vijana kati ya umri wa miaka 18 hadi 35 ni 15,650,998 (vijana wa kiume ni 7,804,845 na kike ni 7,846,153, huku watu wenye ulemavu wakiwa ni 13,211 na kati yao, 2,223 wana ulemavu wa macho, 4,911 ulemavu wa mikono na 6,077 wana ulemavu wa aina nyingine.

"Tume itatumia jumla ya vituo vya kupigia kura 80,156, kati ya vituo hivyo, Tanzania Bara itakuwa na vituo 79,670 na Zanzibar vituo 485, vile vile tume itatumia vituo 1,412 vya ZEC kwa upande wa Tanzania Zanzibar na katika kila kituo kati ya hivyo, kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.

"Baadhi ya vifaa vimepokelewa katika maghala ya tume na baadhi vimesambazwa katika halmashauri nchini, maandalizi ya kupeleka vifaa kwa ajili ya mafunzo kwa watendaji wa vituo vya uchaguzi katika halmashauri yananaendelea, ambapo jumla ya watendaji wa vituo 320,620 watasimamia na kuendesha zoezi la upigaji kura vituoni," amesema.

Akichangia hoja, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) mkoa wa Shinyanga, Richard Mpongo amesema kuwa kundi lao ndilo lenye mahitaji kuliko mengine, hivyo akashauri tume kuona namna ya kutoa nafasi za viti maalum kwa watu wenye ulemavu kwa sababu kiuhalisia hawawezi kupambana na watu wasio na ulemavu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani mkoa wa Shinyanga, Barulisa Khamis ameshauri viongozi wa dini kupewa kipaumbele kwenye zoezi la upigaji kura kama ilivyo kwa makundi maalum, kwani haipendezi kupanga foleni bali wapewe nafasi ya kupiga kura na kuondoka ili wakatoe huduma zingine kwenye jamii.

Pia Mdau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga kutoka asasi za kiraia, Jonathan Manyama ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la Thubutu Afrika, aliiomba tume hiyo kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuondoa upotoshaji wa baadhi ya watu kwenye majukwaa kuhusu tarehe na siku ya upigaji kura.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Oktoba 2,2020 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna katika Manispaa ya Shinyanga. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akisisitiza jambo kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020 kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020 kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakifuatilia mada mbalimbali kwa umakini wakati wa mkutano huo.
Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga. kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Chama cha Watu wenye Ualbino Mkoa wa Shinyanga, Lazaro Anael (kulia), akitoa msaada wa lugha ya alama kwa watu wenye ulemavu wa kutosikia (Viziwi) waliohudhuria mkutano wa wadau wa Uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga, Soud Suleiman Kategile akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la KKKT Shinyanga na Simiyu,Trafaina Nkya akichangia hoja.
Padri Simon Maneno kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani mkoa wa Shinyanga, Sheikh Balilusa Khamis akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mdau wa uchaguzi Jonathan Kifunda Manyama kutoa shirika la Thubutu Africa Initiatives akichangia hoja.
Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi mkoa wa Shinyanga, Justine Shindai akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Shinyanga, Anderson Lyimo akichangia hoja kwenye mkutano huo.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano huob.
Baadhi ya wadau kutoka kundi la wanawake na vijana wakifuatilia ajenda mbalimbali kwenye mkutano huo.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga kutoka kundi la waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC), Greyson Kakuru (kulia) akifuatilia mada mbalimbali kwenye mkutano huo.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.
Baadhi ya viongozi wa dini na wazee katika mkoa wa Shinyanga wakiwa sehemu ya kikao hicho leo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard na wageni wa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa dini waliohudhuria kikao hicho.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria kikao hicho
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard pamoja na wageni wa meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard na wageni wa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka kundi la walemavu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard na meza kuu katika picha ya pamoja na wadau kutoka kundi la asasi za kiraia.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments