Header Ads Widget

KATAMBI ASHINDA UBUNGE SHINYANGA MJINI KWA KURA 31,831, CCM YASHINDA KATA ZOTE

Patrobas Katambi

Na Damian Masyenene, Shinyanga
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ametangazwa mshindi wa ubunge baada ya kupata kura 31,831.

Katambi ametangazwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho leo Oktoba 29, 2020 na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi, huku mpinzani wa karibu wa Katambi, Salome Makamba wa Chadema akiambulia nafasi ya pili kwa kupata kura 16,608.

Wagombea wengine katika kinyang'anyiro hicho walikuwa ni Godwin Makomba (ACT Wazalendo) aliyepata kura 883, Charles Shigino wa NCCR Mageuzi (133), Abdallah Issa Sube (Demokrasia Makini) kura 99, Yahya Khamis wa UDP kura 69 na Malengo Elias wa TLP kura 65.

Msimamizi huyo wa uchaguzi ameeleza kuwa katika zoezi la upigaji kura Jimbo la Shinyanga Mjini, wapiga kura walioandikishwa ni 120,944, idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni 50,453, idadi ya kura halali ni 49,688 na zilizo haribika ni 765.

Katika hatua nyingine, Mwangulumbi amebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti vyote vya udiwani katika kata 17 za jimbo hilo, ambapo kabla ya uchaguzi huo ni Kata nne za Kitangiri, Ndala, Ngokolo na Ibadakuli zilikuwa upinzani kupitia Chadema.

Post a Comment

0 Comments