Header Ads Widget

WAZIRI MKUU AYAVUNJA MAKUNDI YA CCM


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amevunja makundi ya wanachama wa CCM walioomba uteuzi wa kuwania Ubunge katika jimbo la Monduli mkoani Arusha na kuwataka washirikiane katika kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo, wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Monduli, kwenye mkutano wa kampeni za CCM za kumuombea kura Rais Dkt Magufuli pamoja na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani wa CCM.

"Kazi iliyonileta hapa ni kuwaomba kura wana Arusha na wana Monduli, naomba kura zenu zote bila ya kujali itikadi za vyama vyenu, tumpigie kura Mheshimiwa Rais Magufuli na mgombea Ubunge Fredrick Lowassa na wagombea wote wa udiwani kupitia CCM", amesema Waziri Mkuu.

Mbali na hayo Waziri Majaliwa amesema Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, imeweka msisitizo kwa Serikali kuleta mageuzi ya utalii, kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwa na uhakika wa chakula na kujitegemea kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi.