Header Ads Widget

WASHITAKIWA 147 WAFUTIWA KESI DPP AWAONYA KURUDIA MAKOSA AITAKA JAMII KUWAPOKEA


Mkurugenzi wa Mashtka nchini Biswalo Mganga akizungumza wakati wa ufunguzi wa jengo la ofisi ya taifa ya mastaka wilaya ya Kahama ambapo amesisistiza juu ya suala  la ushirikiano kati ya ofisi yake na mamlaka zingine wanazofanya kazi kwa pamoja.

Na Salvatory Ntandu na Stella Ibengwe 

Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Nchini (DPP) Biswalo Mganga  amewafutia Mashtaka washitakiwa  147 katika Mkoa wa  Shinyanga  ambao walikuwa wakisubiri kesi zao kutajwa Mahakamani na kuwataka kuwa raia wema katika maeneo wanayoishi sambamba na kutojihusisha na vitendo vya uhalifu.

Akizungumza  mapema Septemba 3,20202 Mjini Kahama katika Hafla maalumu ya uzinduzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ya Wilaya hiyo Biswalo amesema wamezingatia vigezo vikuu viwili  vinavyotakiwa na kwa mujibu wa sheria ambavyo ni pamoja na kuzingatia  Maslahi ya taifa na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha katika mashauri hayo.

Wengine tumewafutia mashitaka kutokana ushahidi uliopo katika mashauri yao kutojitosheleza ambao utawezesha kuwatia hatiani pasipo kuacha shaka yeyote,pamoja na kuangalia maslahi ya taifa katika utendeshaji wa kesi hizo,”alisema Mganga.

Amesema kuwa miongoni makosa yaliyofutwa kwa mahabusu hao ni pamoja na Mauaji,kupigana,kukamatwa na gongo,na kuingia kwa Jinai(Uvamizi wa migodi bila ya kuwa na vibali) ambayo yalikuwa bado hayajatolewa maamuzi.

Awali akitoa Taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Mashitaka ya Mkoa wa Shinyanga Naibu Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya shinyanga Ramli Mbuya amesema kuwa wilaya ya Kahama yenye Halmashauri tatu za Msalala,Ushetu na Kahama Mjini zina matukio mengi ya Uhalifu ikilinganishwa na maeneo mengine katika mkoa huo.

Wastani wa Mshauri mbalimbali ya Jinai yanayofunguliwa katika ofisi yetu ya mkoa kwa mwaka  kutoka kahama ni 1300 ndio maana tumelazimika kuongeza Mahakimu wawili ili kuhakikisha wanasikiliza mashauri hayo kwa wakati hivyo kufunguliwa kwa ofisi hiihapa kahama ni sera ya nchi na kitaifa ya kwamba wananchi wapate huduma mahali walipo ili  kutasaidia kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la kahama,”amesema Mbuya.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali Mkoa wa Shinyanga Bi Magreth Ndaweka amesema kuwa awali wananchi walipaswa kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 100 kuafuata huduma  hizo mjini Shinyanga hali iliyokuwa ikichangia mashauri mengi kuchelewa kusikilizwa hivyo uanzishwaji wa ofisi ya mashtaka wilaya ya Kahama utakuwa sehemu ya kupunguiza malalamiko na msongamno magerezani.

“hii itasaidia wananchi kupunguza gharama za wananchi kwenda sehemu nyingine kutafuta huduma zetu  hii ilikuwa inatokana na  wilaya hii kuwa na halmashauri tatu za kahama mji, Ushetu na msalala hivyo walikuwa wanapata wakati mgumu sana”

Mmoja wa wakazi wa Mji wa kahama aliyeshuhudia kufunguliwa kwa huduma za kimashitaka katika eneo hilo  Wilfred Birago ameipongeza serikali kupitia Ofisi ya taifa ya mashitaka kwa kuona umuhimu na uhitaji wa huduma hiyo na kuamua kuwasogezea kwani walikuwa wakiitafuta umbali mrefu hali iliyokuwa ikichangia haki kuchelewa

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amoni Mpanju amesema kuwa katika ziara waliotembelea Magereza katika Mikoa ya Shinyanga na Geita washitakiwa wengi ni wa makosa ya mauaji yatokanayo na Ramli chonganishi yatokanayo na migogoro ya kifamilia.

“Inasikitisha kwa karine hii bado kunawatu wanaimani za kishirikina serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu watakaobainika kufanya shughuli za ramli chinganishi sambamba na wanaotekeleza mauaji hayo,”amesema Mpanju.
Sambamba na hilo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria Mpanju amewaagiza wakurugenzi wote nchini kuhakikisha kila wanapojenga majengo ya Umma kutenga vyumba viwili kwa ajili ya Ofisi ya Taifa ya Mashitaka ili kurahisisha utendaji kazi na utoaji wa haki kwa wananchi.
Mwisho.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju akiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Mashitaka Wilaya ya Kahama kwa ajili y ufunguzi wa ofisi hiyo 
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju akisaliamiana na mkuu wa wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita  Mh. Martha Mkupasi wilayani Kahama 
 baadhi ya wakazi wa Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wakiendeleza kusikiliza maelezo ya viongozi toka ofisi ya taifa ya Mashitaka waliohudhuria ufunguzi wa ofisi ya wilaya ya Kahama mapema septemba 3 

 Wajumbe wa kamati za ulinzi na Usalama toka Wilaya za Kahama,Mbogwe na Bukombe wakiwa wameketi kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa ofisi ya taifa ya Mashitika katika wilaya Kahama 

  Viongozi mbalimbali wa wilaya za Mbogwe na Bukombe wakiwa na Naibu Katibu Mkuu wizara ya  Katiba na Sheria Amon Mpanju pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) iswalo Mganga wakiwa wamesimama kwa maombi yaliyokuwa yakiongozwa wa dini

 Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP)Biswalo Mganga akiteta jambo  na Naibu katibu Mkuu wizara ya katiba na Sheria Amon Mpanju wakati wa Uzinduzi wa ofisi za mashtiaka wilaya ya Kahama.

 Wananchi wa Wilaya ya Kahama wakiendelea kusikiliza viongozi mbalimbali wa serikali 

 Mzee Wilfred Birago akizungumza kwa niaba ya wazee wa wilaya hiyo juu ya umuhimu wa uwepo wa ofisi ya mashitka wilayani humo 

 Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi wanyamapori nchini William Kitedi akizungumza katika hafla hiyo ya ufunguzi wa ofisi  ya taifa ya mashitaka 

 Naibu Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya shinyanga Ramli Mbuya  akizungumzia hali ya  kesi ambapo amesema kuwa wilaya ya kahama  pekee upokea mashitika 900

 Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Bi Martha Mkupasi akieleza namna wanavyosafiri umbali mrefu kufuata huduma za kimahakama kati ya  Mbogwe na Kahama pia Ushirimbo ambao ni Mzunguko wa zaidi ya kilomita 200 hali inayowapa wakati mgumu 

 Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza mbele ya hadhara mjini Kahama

 Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka nchini Edson Makalllo akieleza namna ambavyo ifisi hiyo ya wilaya ya Kahama itakavyotumika kuendesha mashitika 


 Mkurugenzi wa Mashitika nchini Biswalo Mganga akifurahia jambo na watumishi aliyowateua kubaki katika ofisi hiyo

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa ofisi ya mashitaka wilaya ya Kahama 

 jengo linalotumika kama ofisi ya mashitaka ya wilaya Kahama 


 Mkuu wa Mashitaka Mkoa wa   Shinyanga Magreth Ndaweka akiwa katika picha ya  pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo 

 Watumishi wa ofisi ya taifa ya mashitaka toka mikoa ya Shinyanga,Geita na Simiyu na Mara wakiwa katika picha ya pamoja 

 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na  naibu katibu mkuu wa wizara ya Katiba na sheria Amoni Mpanju 


 Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP)Biswalo Mganga akiteta Jambo na Naibu katibu Mkuu wizara ya katiba na Sheria nchini Amon Mpanju