Header Ads Widget

PICHA: SALOME MAKAMBA ATUA NGOME YA CHADEMA MASEKELO, AMUOMBEA KURA LISSU

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salome Makamba akizungumza eo Jumatano Septemba 9, 2020 na wananchi wa kata ya Masekelo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.  Picha na Kadama Malunde
***
BAADA ya kuzindua kampeni zake za kuomba kura za ubunge jimbo la Shinyanga Mjini jana katika kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, leo Septemba 9, 2020 Mgombea huyo wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba ameendelea na kampeni hizo katika kata ya Masekelo ambayo ilikuwa inongozwa na diwani wa chama hicho tangu mwaka 2010.

Salome Makamba ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, leo akiwa Masekelo amefanya mkutano mkubwa wa hadhara kuomba kura, uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi waliofika kusikiliza sera zake  katika kata hiyo.

Salome amewaomba wananchi wa Shinyanga kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini huku akiwasihi kumchagua Mwandu Mhoja Mayoge kuwa diwani wao sambamba na kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Salome Makamba akizungumza na wananchi wa kata ya Masekelo kwenye mkutano wake wa kampeni kuomba kura ili awe mbunge wa jimbo la Shjinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde
Wananchi wa kata ya Masekelo wakisikiliza sera za Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA, Salome Makamba aliyefika katika eneo lao kuomba kura leo.
Salome Makamba akiwaeleza sera na kuwaomba wananchi wa kata ya Masekelo leo.
Wananchi wa kata ya Masekelo wakisikiliza sera za CHADEMA katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi ulioongozwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Salome Makamba.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba, akimnadi Mgombea Udiwani kata ya Masekelo,  Mwandu Mhoja Mayoge.
Juma Protas, Meneja Kampeni wa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga kupitia CHADEMA, Salome Makamba akimnadi mgombea udiwani kata ya Masekelo Mwandu Mhoja Mayoge (kushoto).
Mgombea udiwani kata ya Masekelo, Mwandu Mhoja Mayoge akiwaomba wananchi wa kata ya Masekelo wamchague kuwa diwani wa kata hiyo.
Kada wa CHADEMA Joseph Kasambala ' kutoka timu ya Ushindi ya Salome Makamba' akiwaombea kura wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia chama hicho. 
Wananchi wa kata ya Masekelo wakisikiliza sera za CHADEMA katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi ulioongozwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga, Salome Makamba.
Aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu kata ya Masekelo, Zainab Heri (CHADEMA) akiwaombea kura wagombea wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu 2020.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini, Samson Ng’wagi akiwanadi wagombea wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu 2020.
Wananchi wa kata ya Masekelo wakisikiliza sera za CHADEMA katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi ulioongozwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba ‘ Ng’wana O Shimba’.
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini, Hamis Ngunila akiwaombea kura wagombea wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu 2020.
Wananchi wa kata ya Masekelo wakisikiliza sera za CHADEMA katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi ulioongozwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba ‘ Ng’wana O Shimba’.
Wananchi wa kata ya Masekelo wakisikiliza sera za CHADEMA katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi ulioongozwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba ‘ Ng’wana O Shimba’.
Wananchi wa kata ya Masekelo wakisikiliza sera za CHADEMA katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi ulioongozwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba ‘ Ng’wana O Shimba’.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba ‘ Ng’wana O Shimba’ akipokea michango ya wanachama wa CHADEMA na wananchi wa Masekelo kuchangia Kampeni za uchaguzi CHADEMA.
Awali Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga kupitia CHADEMA, Salome Makamba akiwasili katika kata ya Masekelo leo Jumatano Septemba 9,2020 kwa ajili ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wake wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020.