Header Ads Widget

MAMA SAMIA: MLIOSHINDWA KURA ZA MAONI MSILETE NONGWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan, amewataka wanachama waliojitokeza kuwania nafasi za Ubunge na Udiwani wasikisuse chama baada ya kushindwa katika kura za maoni.

Mama Samia amesema hayo leo Septemba 8, 2020 wakati akihutubia wananchi wa Kigamboni alipokuwa akimuombea kura Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt John Magufuli pamoja na mgombea Ubunge wa Jimbo hilo na Madiwani wake.

Mama Samia amesema wakati wa mchakato wa kura za maoni watia nia walikuwa wengi, lakini anashangaa baadhi ya maeneo haoni wakishirikiana na wenzao waliopata nafasi ya kukiwakilisha Chama.

"Mlijitokeza wengi Kigamboni kuwania Ubunge Jimbo la Kigamboni, lakini leo siwaoni mkija kuungana na mgombea aliyepitishwa”, amesema Mama Samia.

"Kwenye Urais mliona watu walivyojitokeza lakini baada ya kupata wagombea wawili wa Zanzibar na Tanzania Bara, wote ambao kura hazikutosha waliwaunga mkono wagombea waliopita, hivyo Wabunge na Madiwani mliopungukiwa kura msiwe na nongwa kitumikieni chama tafadhali", ameongeza Mama Samia.