Header Ads Widget

DPP AFUTA MASHTAKA 95 YA WASHITAKIWA MKOANI GEITA ATAKA WAKAWE RAIA WEMA


Mkurugenzi wa Mashtaka nchini  Biswalo Mganga leo Septemba 06 ,2020 amewafutia Mashtaka washitakiwa 95  waliokuwa katika Gereza la  Mkoa wa Geita.

Biswalo amewafutia Mashtaka hayo  baada ya kutembelea na kuzungumza na baadhi ya washtakiwa ndani ya Gereza la Mkoa wa Geita kisha kujionea hali halisi ya uendeshaji wake, ambapo pia Biswalo amekagua na kusikiliza  Mahabusu na wafungwa walioko ndani ya Gereza hilo.

Mkurugenzi huyo wa mashtaka nchini(DPP) ametaja sababu mbalimbali  zilizopelekea kuwafutia mashtaka ikiwa ni pamoja na wale wenye makosa madogo,ushahidi  kuwa hafifu Wazee na Vijana chini ya umri wa miaka kumi na nane(18) baada ya kuwahoji.

Awali akizungumza na washtakiwa hao Mkurugenzi wa Mashtaka amewataka kuacha kujihusisha na vitendo viovu  vitakavyowafanya kuingia  tena Gerezani  badala yake wakawe mfano bora kwa kuwa raia wema  kwa jamii wanayokwenda kuishi nayo. 

Katika ziara hiyo ya kutembelea na kukagua gereza hilo mkurugenzi mkuu wa mashtaka nchini  Biswalo Mganga ameongozana  na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na  Usalama Mkoa wa Geita.
Mwonekano wa  Gerezani la Wilaya ya Geita Mkoani humo lililotembelewa na mkurugenzi wa Mashitaka nchini DPP Biswalo Mganga mapema hii leo Septemba 6,2020 
 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akizungumza na maafisa wa jeshi la Magereza,Kamati ya Ulinzi na usalama ya  Mkoani Geita kabla ya kutembelea na kukagua Gereza la Wilaya ya Geita 
Wajumbe wa kamati ya Usalama pamoja na Maafisa wa magereza wakiendelea kusikiliza ujume wa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP Biswalo Mganga