Header Ads Widget

MGOMBEA UBUNGE CCM KAHAMA ASEMA MJI HUO KUWA WA KISASA BAADA YA KILOMITA 23 ZA LAMI KUTANDAZWA


Mgombea Ubunge  Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba aliyeko juu ya Jukwaa akiendelea kunadi sera zake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kampeni jimboni humo 

Picha na SPC 

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  Jimbo la Kahama Mjini  Jumanne Kishimba (Maarufu Profesa Kishimba) amewaomba wakazi wa jimbo hilo kumchagua ili kwenda kukamilisha mipango ya maendeleo aliyoanzisha kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ikiwemo kuendelea kutatua changamoto za sekta ya Afya,Masoko na Barabara 

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kunadi sera za (CCM) wakati wa Uzinduzi wa Kamapeni za jimbo hilo uliofanyika katika  kata ya Kagongwa Kishimba amesema kuwa tayari benki ya Dunia imetoa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Kilomita 23 za Barabara katika Mji huo.

"Naomba Niwaambie kama ambavyo amekwisha sema Naibu waziri wa Ujenzi Ndg. Kwandikwa tumepata mradi wa  toka benki ya Dunia ambao watatujengea Stendi  mpya na ya kisasa,Barabara Kilomita 23 na mitaro yote ya mji hivyo Kaham itakuwa inang'aa Muda wote"

Akizungumzia suala la afya Mgombea huyo kupitia CCM anayetetea kiti chake amesema kuwa alipoingia Mwaka 2015 jambo la Kwanza kushughulikia ilikuwa ni sekta yta Afya ambayo ni changamoto kubwa kwa kina mama ambapo alikamilisha majengo ya zahanati zote zilizokuwa zimejengwa ili kusogeza huduma kariu zaidi na wananchi. 

"Mimi  nilipoingia tu kwenye Madaraka nguvu zangu zote nilihamishia kwenye zahanati kwanza ngoja niwaambie umaskini mimi naujua na nimeukulia hapa hapa Kagongwa  na nimefanya biashara aina mbalimbali baada ya kuchaguliwa kitu cha kwanza kukimbilia  ni huduma ya afya mimi baba yangu alifariki nikiwa na miaka 3 hivyo nililelewa na Shangazi yangu kwa hiyo maisha yote nayafahamu ndiyo maana mara baada ya kuchaguliwa nilikimbilia kwenye sekta ya afya"

Aidha Kishimba ameongeza kuwa mara baada ya kuchaguliwa 2015  alitumia zaidi ya shilingi milioni 40 kutoka mfukoni kwake kununua vitanda kwa ajili ya kina mama kujifunguliwa huku akitolewa mfano wa hospitali ya mji kahama iliyokuwa na vitanda nane huku ikizalisha kina mama 40 hadi 70 kwa siku jambo lililomsukuma kununua vifaa hivyo ikiwemo magodoro,vitanda na mashine za kusaidia kupumua kwa watoto njiti.

Awali akiomba kura kwa wakazi wa kahama Mgombea Ubunge jimbo la Ushetu  Elias Kwandikwa ambayeni Naibu Waziri wa Ujenzi amesema kuwa mradi wa benki ya dunia umefikia hatua za mwisho na muda si mrefu wataanza utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo kilomita 23 za lami pamoja na kilomita 5 katika mji wa uwekezaji zongomela maarufu Dodoma

"Mnaona tumeenda kwenye uchumi wa kati sasa naomba niwaambie tu watu wa kahama  kuwa kwa sasa tuna mpango wa kuboresha uwanja wa ndege kwa kuongeza mita mia tano(500) zitakazosaidia kuongezeka miruko ya ndege na kupeleka bombadia kutua na kukuza uchumi wa Kahama hivyo chagueni wagombea wa CCM "

Katika hatua nyingine kwandikwa amesema kuwa serikali iko katika mchakato wa kujenga reli toka Isaka  kwenda Keza ambapo itachangia kujengwa kwa stesheni Kahama Mji hivyo uwekezaji utaongezeka,kipato kitakuwa na huduma za usafiri zitaongeza na kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejitahidi kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kukuza uchumi wa nchi kutoka kiwango cha chini hadi kati hali itakayochangia jamii kuendelea kupata huduma bora za kijamii.

Mabala ameendelea kugusia suala la  amani kwa vijana kudumisha kwani maendleo ya taifa lolote uletwa na amani umoja na mshikamano ambapo amewaomba vijana wa chama hicho pamoja na waombea wa vijana vingine kuendesha kampeni za kistarabu.

"Niwaombe ninyi vijana wa chama cha mapinduzi  akikisheni mnafanya kampeni za kuistaarabu kwanza nimeshasikia kuna watu wamechana mabango yetu  nanyi msiende kulipiza tafadhali mkiona au mkimbaini mpelekeni kwenye vyombo vya dola lakini sitaki watu wafike huko nyie msifanye fujo"

Nao baadhi ya Wakazi wa jimbo la Kahama mji wamesema kuwa wanayo matumaini makubwa toka kwa mgombea huyo anayetetea kiti chake ambapo wamesema kuwa tayari amekwisha onyesha moyo wa kuisadia jamii

Maria Kashinje na Sofia Maiko ni baadhi ya wakazi wa mji ho wamesema kuwa kwa sasa upatikanaji wa huduma za afya na nyinginezo zimeongezeka kwa kiwango kizuri kitendo kinaonekana ni utendaji mzuri wa mgombea huyo 

Mwenyekiti wa (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba Maarufu Profesa kishimba wakati wa uzinduzi wa Kampeni kata ya Kagongwa nje kidogo  ya mji wa Kahama
Wa kwanza kushoto mwenye shati la Njano ni Mgombea Ubunge jimbo la Ushetu Wilayani Kahama ambaye pia ni Naibu waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akicheza ngoma ya asili maarufu bachwezi wakati wa uzinduzi huo 
mwenyekiti wa (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na Wakazi wa Kahama mji kata ya Kagongwa   
Mwenyekiti wa (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akimnadi Mgombea Udiwani kata ya Kagongwa  

Baadhi ya  Wagombea nafasi ya udiwani kahama mji wakiwa mbele ya wapiga kura  
Baadhi ya  Wagombea nafasi ya udiwani Ushet  waliofika kushudia kuzinduliwa kwa kempani jimbo la kahama mji   

 Aliyekuwa kuwa mbunge wa jimbo la Kahama na Mtia nia wa ubunge  kwenye mchakato uliopita James lembeli akizungumza na wanachama pamoja na wapiga kura wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo eneo la kagongwa 

Mgombea Ubunge  Viti maaalum kwa tiketi ya CCM Mkoa wa Shinyanga Lucy Mahenga akiendelea kuomba kura za Rais, wabunge na udiwani. 
Mgombea Ubunge  Viti maaalum kwa tiketi ya CCM Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akiendelea kuomba kura za Rais, wabunge na udiwani. 

 Mgombea Ubunge  Viti maaalum kwa tiketi ya CCM Mkoa wa Shinyanga Dr Mnzava  akiendelea kuomba kura za Rais, wabunge na udiwani. 

  Mgombea Ubunge  Viti maaalum kwa tiketi ya CCM Mkoa wa Shinyanga Dr Mnzava akiendelea kuomba kura za Rais, wabunge na udiwani wakati amepiga magoti kwa wanananchi ikiwa ni ishara ya unyenyekevu 

Mgombea Ubunge jimbo la Ushetu Wilayani Kahama ambaye pia ni Naibu waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na wakazi wa Kagongwa  wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM Kahama Mji  

 Viongozi mbalimbali wa chama chamapinduzi Mkoa wa Shinyanga na wilaya ya Kahama wakiwa wameketi na kufautilia burudani zinazoendelea 
 Sehemu ya wakazi wa Kahama Mji wakifuatilia hotuba za wagombea 
 Sehemu ya wakazi wa Kahama Mji wakifuatilia hotuba za wagombea 

 baadhi ya Watoto nao wamefika kusikiliza hoja za wagombea ili wafikishe ujumbe kwa wazazi  wao 
wa kwanza kushoto ni mke wa Profesa  Jumanne Kishimba akiomba kura kwa ajili ya Mumewe na madiwani ili kwenda kutetea haki za wanawake 
burudani pia ilikuwa sehemuya uzinduzi huo