Header Ads Widget

JAJI MARK BOMANI AFARIKI DUNIA

Jaji Mstaafu Mark Bomani

Jaji Mstaafu Mark Bomani ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital hii leo Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, amethibitisha na kusema kuwa Jaji Mstaafu Mzee Bomani alilazwa hospitalini hapo kwa siku 24.

"Jaji Mstaafu amefia hapa Muhimbili, amefariki majira ya saa 4:00 usiku wa kuamkia leo, na alikuwa hapa hospitalini kwa siku 24", amesema Aligaesha.

Jaji Mstaafu Mark Boman alizaliwa Oktoba 22 mwaka 1943, huko Wete, Pemba, Visiwani Zanzibar na aliwahi kuhudumu kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania kuanzia mwaka 1965 hadi 1976. 
CHANZO: EATV