Header Ads Widget

DC MBONEKO AKAGUA MIRADI YA ELIMU MANISPAA YA SHINYANGA ATAKA KUKAMILIKA UJENZI WA MADARASA NA VYOO KABLA YA SEPTEMBA 30


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mh Jasinta Mboneko na kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya wakikagua ujenzi wa Madarasa mawili katika Shule ya  Msingi Mwalugoye.

Mapema  Septemba 16 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko Amefanya ziara katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari  zilizopokea fedha toka serikalini kwa lengo la kuongeza miundombinu ya Madarasa na Matundu ya Vyombo Manispaa ya  Shinyanga.

  amesema kuwa serikali imetoa fedha zaidi ya Shilingi Milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na matundu ya vyoo kwa lengo la kupunguza adha na kero kwa watoto wa shule

Akiwa shule ya Msingi Mwihando Kata ya Old Shinyanga Mboneko amekagua ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo ambapo amemtaka fundi anayetekeleza mradi huo kukamilisha kwa wakati ili kuondoa kero kwa wanafunzi wa shule hiyo

“Ili iwe kwa wote wanaotekeleza ujenzi wa miundombinu ya Serikali hususani kwa shule zilizopata fedha hakikisheni mnakamilisha ujenzi huo kwa wakati na ifikapo Septemba 30 miundombinu hii ianze kufanya kazi na  ndiyo lengo la serikali kwenye hili”

Mboneko ameongeza kwa kusema kuwa  uwepo wa miundombinu hiyo utasaidia  wanafunzi wengi kufanya vizuri katika mitihani yao kutokana na kupunguza adha ya kukaa kwa mrundikano madarasani pamoja na kutumia matundu machache ya Vyoo  ambapo ameendelea kusisitiza suala la ushirikishawaji wa wananchi kwenye miradi ya maendeleo  ili kuisaidia serikali kwani haiwezi tekeleza majukumu yote

“Naomba niwaambie nyinyi viongozi wa Serikali za Vijiji na Kamati za Shule waambie wazazi pia washiriki kwenye miradi hii ya maendeleo kwai tazama serikali imekwisha toa mwanga kwa kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa  madarasa na Matundu ya vyoo basi nanyi jitoeni walau kwa darasa moja kwa sababu hawa ni wetu”

Aidha Mboneko akiwa shule ya Sekondari Old Shinyanga amekerwa na kitendo cha  ujenzi wa Bweni katika shule hiyo kusimama kwa kile kinachodaiwa  kuwa  BOQ yake ilikuwa juu kuliko fedha  iliyotolewa na Serikali kwa ajili  ya Ujenzi huo ambapo serikali muhandisi alitakiwa kubadili BOQ kulingana na fedha iliyotolewa

Akitoa taarifa  ya kusimama kwa Mradi huo  Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Bw  John Tesha amesema kuwa makadirio ya muhandisi wa ujenzi wa manispaa hiyo ilikuwa shilingi milioni 160 ambapo fedha iliyotumwa na serikali ni Shilingi Milioni 80 hali iliyochangia kushindwa kuendlea hadi pale walipobadili BOQ

“Kuhusiana na Kusimama kwa Ujenzi wa jengo la Bweni kwa ajili ya wanafunzi wa Shule hii ni tatizo la BOQ kwa hiyo tumekwisha rekebisha na fundi ataanza nadhani kuanzia muda wowote na litakamilika kwa muda rafiki licha ya kuwa nje ya mkataba”

Nao baadhi ya Walimu wakuu wa Shule zinazotekeleza miradi hiyo ya Vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo  Manispaa ya Shinyanga wakabainisha utekelezaji wa miradi hiyo licha ya kukumbana na changamoto ya ukosefu wa Saruji hali iliyokuwa ikikwamisha miradi kutekelezeka kwa wakati

Anna Alute ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bugoyi A amesema kuwa ujenzi wa Madarsa umefikia hatua ya kufanya Finishingi ikiwemo upigaji wa Lipu huku ujenzi wa matundu ya Vyoo ukifikia asilimia 95

“Kwa Upande wetu sisi Bugoyi A tumejitahidi kusimamia fedha zilizotolewa na Serikali na ningependa kutumia fulsa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutukumbuka na  muda c mrefu matumizi yake yatakuwa tayari na kabla ya Septemba 30 tutakuwa tumekamilisha”

Naye Malale Sawaka Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo amesema kuwa wao wamepokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vitatu vya madarasa pamoja na Matundu ya Vyoo ambapo tayari yako kwenye hatua ya Lipu

“Mpaka sasa zoezi linaloendelea ni upigaji wa Lipu pia tumeshajenga miundombinu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalaumu ili kuwawezesha kupita bila kikwazo kwenye milango  kwa hiyo hatua nzuri tunazidi kuipiga”

Mwarabu  Mwimbili  ni Mwenyekiti wa kamati ya Shule Mwalugoye ameeleza kufurahishwa na hatua iliyochukuliwa na serikali kwa kuhakikisha inatia fedha kwa ajili  ya kutatua kero za watoto wa shule ikiwemo uhaba wa madarasa na upungufu wa matundu ya Vyoo

Kwa upande wake aliyekuwa naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga  John Kisandu ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuleta fedha hizo na kuzigawa kwa shule amabzo zinatekeleza ujenzi wake kwa kutumia mfumo wa fosi akaunti

“Mimi nimefurah kiukweli kuona mambo mazuri kiasi hiki kwani fedha hzi zingeenda kufanya kazi zingine lakini zimeletwa huku hivyo sisi tuna jukumu la kuhakikisha miradi inakamilika na kuleta tija kwa jamii ambapo watoto wetu kukaa kwa msongamano kutapungua”

Mwishooo