Header Ads Widget

VIJANA JIUNGENI NA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA (MGAMBO) ACHENI KUZAGAA MTAANI- DC SHINYANGA


Vijana mbalimbali wanaoshiriki mafunzo ya jeshi la akiba eneo la Old Shinyanga manispaa hiyo wakiwa katika gwaride wakati mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko alipokuwa akiangalia ukakamavu wa vijana hao. 

Vijana 149  toka Manispaa ya Shinyanga wamejiunga na mafunzo ya jeshi la akiba ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wanadumisha amani, umoja na ulinzi wa nchi katika maeneo yao pamoja na kujiimarisha kiafya .

Akifungua mafunzo hayo Agasti 25 Old Shinyanga, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh Jasinta Mboneko amewaasa vijana   hao kuyatumia vema mafunzo hayo ya  kijeshi yanayotolewa   na Jeshi   la wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kuhakikisha wanalinda na kudumisha amani ya nchi pamoja na kujenga mshikamano na umoja

Mboneko amesema kuwa mafunzo hayo ambayo kwa sasa yamefikisha wiki 7 toka kuanza kwake  huku yakitarajia kuchukua miezi minne ambapo  amewataka kuwa na nidhamu wakati wote wa mafunzo na kuacha kusua kusua kwenye mafunzo.

“Kwa hiyo hakikisheni mnahudhuria mafunzo kila siku lakini nidhamu iwe ya hali ya juu mpo kwenye mafunzo tunatizama vitu kuna mnatakavyojifunza darasani  na vingine huku na kila siku nitakuwa napewa taarifa juu ya mafunzo haya kwa hiyo kikubwa ni kuzingatia na kushika  maelekezo mnayopewa na wakufunzi  wenu”amesema Mboneko

Dc Mboneko ameongeza kuwa kwa sasa nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu ambapo suala la amani linapaswa kudumishwa  ambapo amewaasa kuendlea kutunza nidhamu na utulivu pamoja  na kutoa taarifa za hali ya uvunjifu wa amani kwenye maeneo wanakotoka

“Kikubwa ni kuhakikisha kwamba maeneo yetu tunakotoka na kusihi mnakuwa na ninyi ni jicho la serikali na hapa nimeambiwa mko 149 nategemea mmalize wote kwa hiyo niwatahadhirishe msijiingize kwenye vikundi   vya kuhatarisha amani mkono wa sheria utachukua nafasi yake”ameongeza Mboneko 

Naye Mkuu wa mafunzo hayo Kanali Prosper Masawe toka base ya Shinyanga amesema kuwa jukumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni kutoa mafunzo kwa lengo la kusaidia  ulinzi kwenye maeneo wanayotoka pamoja na kuimarisha ulinzi wa nchi hususani nchi  inapoingia kwenye vita huwa tunawatumia katika  mapigano.

“Tunawasihi wale Vijana  ambao wako mtaani asijali umri wala elimu kama hajapata mafunzo ya ulinzi wa nchi yake ni vizuri aje kwenye mafunzo haya ya Jeshi la akiba ambayo tunatumia miezi minne anakuwa tayari ameelewa kwa hiyo hii ni hatua ya nne watakwenda hadi hatua ya kwanza”amesema Kanali Masawe

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo Vijana ambao ni watumishi wa serikali toka Manispaa ya Shinyanga wamesema kuwa jukumu la ulinzi wa nchi ni la kila mtanzania  hivyo mafunzo hayo yatawasaidia katika kupamabana na vitendo vya uharifu kwenye maeneo yao

Ezra Majerenga ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga anayeshiriki kwenyemafunzo hayo amesema kuwa katika kuimarisha ulinzi wa rasimali za nchi lazima uwe na utayari na ukakamvu wa mwili.

Ili uweze kuwa mlinzi mzuri wa rasilimali za nchi unastahili kuwamkakavu na unahitaji mbinu za medani kwa maana ya kujua wapi ambapo maliasili zinatumka vibaya na mifumo ya kuhakiisha kwamba unazilinda kwa kusimamia sheria na taratibu zilizopo” amesema Ezra 

Ufunguzi huo umeambatana na upigaji wa Shabaha kwa askari hao wa Jeshi la akiba,viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa uimarishaji wa suala la ulinzi wa nchi. 
Baadhi ya Vijana wanaoshiriki mafunzo ya jeshi la akiba Manispaa ya Shinyanga wakiwa wamekaa kumsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh Jasinta Mboneko.

Mshauri wa Mgambo wilaya ya Shinyanga Ford Mwakasege (wa Kwanza) kulia akiwa ameketi pamoja na Mkuu wa mafunzo hayo Kanali Prosper Masawe  na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wakifuatilia mazoezi ya upigaji Shabaha kwa vijana wa jeshi la akiba.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwa tayari kwa ajili ya kuanza zoezi la upigaji shabaha eneo la Old Shinyanga 

DC Mboneko akilenga Shabaha wakati wa zoezi la kupiga  shabaha 

Afisa Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bw Beda Vedastus akilenga Shabaha wakati wa zoezi la upigaji shabaha 

Washiriki wa kulenga shabaha wakiongozwa  na  Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi  na usalama  ya wilaya kulenga shabaha 

Mazoezi ya upigaji shabaha yakiendelea 

 Baada ya kupiga shabaha wanafunzi wakiwa wameziba masikio yao 
  
  Mwandishi na Mtangazaji wa kituo cha kijamii cha mjini Shinyanga Bw Isack Eddo akiwa ameziba masikio baada kuhitimisha kulenga shabaha 

Zoezi likiendelea la kulenga na kupiga Shabaha

Afisa Tarafa ya Old Shinyanga naye akilenga Shabaha 
  
Afisa toka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akifurahia zoezi la upigaji Shabaha 

Afisa Uhamiaji wilaya ya Shinyanga  Bw Mwanawima akijiandaa kupiga Shabaha 

  Mwandishi na Mtangazaji wa kituo cha kijamii cha mjini Shinyanga Bw Isack Eddo akiwa akilenga Shabaha 

   Mwandishi na Mtangazaji wa kituo cha kijamii cha mjini Shinyanga Bw Isack Eddo akiwa eneo la shabaha kuona iwapo amepata hata moja

Baadhi ya vijana wanaoshirikimafunzo ya  jeshi la akiba (Mgambo) wakiwa katika Gwaride la pamoja  
Vijana wakiwa wameketi pamoja wakisikiliza ujumbe wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakati wa ufunguzi wa mafunzo.

Zoezi la Upigaji na ulengaji wa Shabaha likiendea 
  



Bw Masunga Mchanga ambaye ni dereva wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga akilenga shabaha 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwachangamsha vijana hao kwa kuimba nyimb za uzalendo 

Mkuu wa wilaya akiendelea na mazoezi  kwa vitendo 

 Wa Kwanza kulia ni Mkuu wa mafunzo ya jeshi la akiba Kanali Prosper Masawe akimkaribisha Mkuu wa wilaya pamoja na kamati yake katika kushuhudia namna vijana wanavyoshiriki mafunzo 
  

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa vijana kujiunga  na mafunzo ya jeshi la akiba. 

 Kanali Prosper Maswe toka base ya Shinyanga ambaye ni mkuu wa mafunzo ya jeshi  la akiba akitoa maelezo ya mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa miezi minne