Header Ads Widget

CRDB YAENDESHA KONGAMANO LA WAFANYA BIASHARA, WAZABUNI NA WAKANDARASI WILAYANI KASULU


 
  Wafanyabiashara, wazabuni na wakandarasi wilayani Kasulu wakifuatilia kongamano lililoandaliwa na Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi


Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako leo Agosti 25, 2020 amefungua kongamano la kibiashara lililoandaliwa na Benki ya CRDB wilayani Kasulu likiwakutanisha wafanya biashara, Wazabuni na wakandarasi wote wilayani Kasulu.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange, Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kasulu, Fatna Laay na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu, Joseph Kashushula.
 Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako akifungua kongamano hilo
 
Akifungua kongamano hilo, Prof. Ndalichako amesema benki ya CRDB ni benki kubwa nchini na ya kizalendo yenye matawi kote nchini, mjini na vijijini kupitia matawi yao zaidi ya 264 Tanzania.

Ndalichako amesema nchi inajivunia benki hiyo kwani kiasi kikubwa inamilikiwa na selikali na watanzania wenyewe, wengi wakiwa ni wenye kipato cha kawaida, pamoja na taasisi mbalimbali za serikali yetu.

"Ni benki bunifu na wakati wote imekuwa mstari wa mbele katika kuboresha maisha ya watanzania kupitia huduma mbalimbali za mikopo, uwekaji wa amana zenye riba nzuri na huduma za kifedha kupitia njia za kidijitali kama vile Simbanking, ATMs, CRDB Wakala, akaunti za watoto maarufu kama JJ na akaunti za kina mama zijulikanazo kama Malkia.
 
 "Kwa niaba ya serikali tunawapongeza na kuwashukuruni sana CRDB kwani mojawapo iliyowekeza kwenye miradi mikubwa ya serikali ikiwemo kutoa mikopo ya Dhamana katika miradi mikubwa ya serikali kama Mradi wa Reli ya kisasa ya SGR na Mradi wa ufuaji umeme wa maji wa Rufiji (RHPP)," amesema.
 
 Prof. Ndalichako ametoa rai kwa wafanya biashara, wazabuni, wakandarasi na wananchi wote wilayani Kasulu na mkoa wa kigoma kuendelea kuitumia benki ya CRDB kwa kufungua akaunti, kuweka amana na kujipatia mikopo mbalimbali yenye riba nafuu. 
 
Meneja biashara wa CRDB Benki kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza katika kongamano hilo

  Wakandarasi, wafanyabiashara na wazabuni wilayani Kasulu wakifuatilia kongamano lililoandaliwa na Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi