Header Ads Widget

UAE YAZINDUA MTAMBO WA KWANZA WA NYUKLIA

Umoja wa Falme za Kiarabu umezindua oparesheni katika kiwanda cha kwanza cha nyuklia kwenye nchi hiyo ya Uarabuni pwani ya ghuba mashariki tu mwa Qatar.

Tayari vipande vidogo vidogo vya nyuklia vimeanza katika moja ya vinuu vyake vinne kwenye mtambo wa Barakah unaotumia teknolojia ya Korea Kusini.
Mtambo huo likuwa unatarajiwa kufunguliwa mwaka 2017 lakini kuliahirishwa kwasababu kadhaa za kiusalama.
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), yenye utajiri wa mafuta inataka kiwanda cha nyuklia cha Barakah kufikia robo ya mahitaji yake ya nishati wakati inageukiwa vyanzo endelevu vya nishati.
Wiki mbili tu zilizopita, UAE ilituma chombo chake katika anga la mbali kwenye sayari ya mihiri moja ya hatua nyingine kubwa iliyopigwa kisayansi katika taifa hilo la ghuba.
UAE pia inawekeza zaidi katika nguvu ya jua - chanzo muhimu cha nishati katika eneo hilo la ghuba.
Baadhi ya wataalamu wa nishati wanahoji uwepo wa kiwanda cha Barakah - ambako kunamaanisha Baraka kwa kiarabu.
Wanasema kwamba nishati ya jua ni safi, rahisi na ndio yenye kuleta tija zaidi eneo hilo katika nchi inayokabiliana na joto la kisiasa na ugaidi.
Mwaka jana Qatar ilisema kwamba mtambo wa nyuklia wa Barakah ni tishio kwa amani na mazingira ya eneo hilo.
Dkt Paul Dorfman, Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa makampuni ya Nyuklia, aliandika mwaka jana kwamba "Wasiwasi wa siasa za kijiografia katika eneo la ghuba linafanya nguvu ya nyuklia kuwa suala tata katika eneo hili kuliko kwengine kokote, kwasababu nguvu mpya ya nyuklia inawezesha kutengeneza silaha za nyuklia".
Katika uchambuzi wake, mwanasiasa huyo mwenye makao yake London pia alionesha wasiwasi wake kwamba usalama wa mtambo wa nyuklia wa Barakah kwa misingi ya kiufundi, kuna hatari ya kusambaa kwa mionzi hatari kwenye eneo la ghuba.
Viongozi wa UAE wamepongeza kuanzishwa kwa mtambo huo wa nyuklia Jumamosi kama ishara ya maendeleo ya kisayansi nchini humo.
Mtambo wa nyuklia wa Barakah uliundwa na Shirika la Nguvu ya Nyuklia la Emirates na Shirika la Umeme la Korea.
Nishati itazalishwa kwa megawati 1,400 za maji ya kwenye vinu vilivyoundwa Korea Kusini kwa jina APR-1400.
Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) - Bodi inayosimamia viwanda vyote vya nyuklia limepongeza mtambo wa Barakah kwenye mtandao wa Twitter, na kusema kuwa kinu cha kwanza kimefikia hatua muhimu ya kwanza ya kutengeneza vipande vya nyuklia.
"Hii ni hatua muhimu katika kufikia oparesheni za kibiashara na uzalishaji wa nishati safi. IAEA imekuwa ikiunga mkono Falme za Milki ya Kiarabu kuanzia mwanzo wa mpango wake wa uzalishaji nyuklia."
Kiongozi mkuu wa Abu Dhabi, Mwana Mfalme Mohammed bin Zayed al-Nahyan, alituma pongezi zake kwa kuandika kwenye mtandao wa Twitter "kufikia hatua hii katika mkakati wa kufikia maendeleo endelevu".
source bbc swahili.