Header Ads Widget

NEC YAWATANGAZA MAKAMBA, NAPE, MNYETI, KABUDI NA WENZAO 14 WALIOPITA BILA KUPINGWA MAJIMBONI

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera ametangaza majimbo 18 ya Uchaguzi ambayo wagombea wake wamepita pekee. Wote ni kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk. Wilson Mahera

Wagombea hao wamepita kama wagombea pekee kutokana na sababu mbalimbali kwa kuzingatia Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na majina yao yatatangazwa kwenye Gazeti la Serikali

Jimbo la Ushetu - Elias John Kwandikwa

Jimbo la Kongwa - Job Ndugai

Jimbo la Gairo - Ahmed Mabkhut Shabiby

Jimbo la Kilosa - Prof. Palamagamba Kabudi

Jimbo la Mvomero - Jonas Van Zeeland

Jimbo la Morogoro Kusini - Kalogereris Innocent

Jimbo la Morogoro Mashariki - Taletale Hamis Shabani

Jimbo la Katavi - Eng. Isaac Aloyce Kamwelwe

Jimbo la Kavuu - Godfrey Mizengo Pinda

Jimbo la Songwe - Philipo Augustino Mulugo

Jimbo la Bukene - Zedi Selemani Jumanne

Jimbo la Nzega Vijijini - Dr. Kigwangala Hamis Andrea

Jimbo la Ruangwa - Kassim Majaliwa Majaliwa

Jimbo la Mtama - Nape Moses Nnauye

Jimbo la Namtumbo - Vita Rashid Kawawa

Jimbo la Butiama - Sagini Jumanne Abdallah

Jimbo la Misungwi - Alexander Pastory Mnyeti

Jimbo la Bumbuli - January Yusuf Makamba