Header Ads Widget

KOCHA MSERBIA WA YANGA ATUA NCHINI, KUIONGOZA TIMU KESHO

Kocha Mpya wa timu ya Yanga, Mserbia Zlatko Krmpotic




Jana Agosti 28, 2020 Uongozi wa klabu ya Yanga  ulimtangaza kocha mpya atakaekinoa kikosi chao kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara ambao utaanza rasmi Septemba 6, mwaka huu.
Yanga ilimemtangaza kocha huyo kupitia kwa Mjumbe wa Kamati ya Usajili ambaye pia ni Mkurugenzi Uwekezaji wa Kampuni ya GSM inayoidhamini klabu hiyo Injinia Hersi Said.

Injinia Said amemtangaza kocha Zlatko Krmpotic raia wa Serbia ambaye ana uzoefu na soka la Bara la Afrika, huku akipita kwenye klabu yenye mafanikio katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, TP Mazembe ya DR Congo.


Kocha mpya wa klabu ya Yanga SC, Zlatko Krmpotic akiwa na Afisa Habari wa klabu, Hassan Bumbuli baada ya kutua rasmi nchini tayari kwa kuanza kibarua chake.


KAZI YA UKOCHA

Kocha Zlatko amefanya kazi katika vilabu kadhaa kwenye nchi 12 tofauti duniani.

Nchi hizo ni Serbia akiwa na klabu za AIK Bačka Topola, OFK Beograd, na Obilić. Sweden (Degerfors IF) , Macedonia (Sloga Jugomagnat), Uturuki (Ankaragücü ), Ugiriki (Paniliakos), Kupro (Nea Salamis), Kazakhstan (Kairat), Kuwait (Kazma), DR Kongo (Don Bosco) na TP Mazembe kama kocha msaidizi, Zambia (ZESCO United), Botswana (Jwaneng Galaxy), na Kusini Afrika (Royal Eagles).

Pia kocha Zlatko amewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 19 Serbia na Montenegro mwaka (2005), na baadae alikabidhiwa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 19 cha Serbia kuanzia mwaka 2007-2008.

MAFANIKIO
Akiwa na klabu ya Red Star Belgrade kama mchezaji, Zlatko alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Yugoslavia *Yugoslav First League* mara tatu na hiyo ilikuwa msimu wa 1979–80, 1980–81 na 1983–84.

Akatwaa ubingwa wa Yugoslav Cup kwama mchezaji mara mbili msimu wa 1981–82 na 1984–85.

MAFANIKIO YAKE KIMATAIFA
Alikuwa sehemu ya kikosi cha Yugoslavia chini ya umri wa miaka 21, kilichotwaa ubingwa wa UEFA mwaka 1978

Msimu wa 2016-2017 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Ligi ya DR Congo.

Msimu wa 2017-2018 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Ligi ya Zambia (Zambian Superleague)

Msimu wa 2018-2019 alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Ligi ya Botswana.

Shirikisho la soka Afrika CAF lilimtangaza kuwa kocha bora wa barani hilo msimu wa 2017-2018.