Header Ads Widget

RAIS DR JOHN MAGUFULI ATAKA KAMPENI ZA CCM KUZINDULIWA DODOMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amesema kuwa anatamani kampeni za chama hicho kuanzia Jijini Dodoma,  ambapo makao makuu Nchi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo mapema hii leo  wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho Jijiini Dodoma baada ya kuchukua fomu ya Urais katika   Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Rais Magufuli amesema kuwa wakati anaingia madarakani   mwaka 2015 amekuta  vijiji vyenye umeme vikiwa elfu tatu (3000) ambapo amejitahidi na kufikisha Vijiji Elfu tisa (9000) mara mbili  ya vile alivyovikuta.

Ameongeza kuwa  iwapo atarejea  tena madarakani kwa kipindi kilichosalia cha miaka mitano 2020-2025  atahakikisha vijiji vyote nchini vipatavyo  elfu kumi na mbili (12000) vinafikiwa na umeme.