Header Ads Widget

RASMI: ACT WAZALENDO YAWAPITISHA MEMBE NA MAALIM SEIF KUGOMBEA URAIS


Mgombea Urais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (Kushoto). Kulia ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bernard Membe.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, wamempitisha Mshauri Mkuu wa chama hicho, Bernard Membe kupeperusha bendera ya chama hicho katika kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu. 

Maamuzi hayo yameamuliwa leo Agosti 5, 2020 kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Membe ameibuka mshindi kwa kupata kura 410 kati ya kura 420.

Aidha Wajumbe wa mkutano huo pia wamempitisha Mwenyekiti wa chama, hicho Maalim Seif Sharif Hamad, kuwa mgombea Urais wa Zanzibar, baada ya kupata kura 419 kati ya kura 420.