Header Ads Widget

MRADI WA PETS SHINYANGA WAPONGEZWA KUIBUA WATOTO WENYE ULEMAVU KUSOMA



Na Patrick Mabula-Shinyanga
Mradi wa kufuatilia fedha zinazotolewa na serikali (PETS) katika shule za msingi zenye watoto mchanganyiko na wenye mahitaji maalumu (walemavu ) unaotekelezwa na wenye ulemavu wa wasioona (vipofu) mkoani Shinyanga umepongezwa kutokana na mafanikio mazuri miongoni mwa jamii.

Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Elimu Kata ya Tinde Halmashauri ya Shinyanga Vijijini, Justus Bilago alipokuwa akizungumza na walimu wakuu, watumishi wa umma na wenyeviti wa vijiji wa kata zilipo shule za msingi zenye watoto jumuishi wanaosoma na wenye ulemavu zinazopatiwa fedha hizo.

Alisema mradi huo umeanza kuleta matokeo chanya miongoni mwa jamii na kuanza kuwa na mwamko wa kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu waweze kupata elimu kwa sababu hiyo ni haki yao ya msingi na kuacha tabia ya kuwaficha.

Bilago alisema tangu mradi huo uanze mwaka 2019 kumekuwepo na ongezeko la watoto wenye ulemavu mbalimbali kupelekwa na kuandikishwa katika shule za msingi zinazopatiwa fedha za matumizi kwa walemavu hao za kuboresha mazingira ya kusoma.

Alisema mradi huo unaendelea kuwapa mwamko jamii ambayo imeanza kuachana na mira na desturi zilizopitwa na wakati za kuwaficha watoto walemavu na kwa sasa wanawapeleka shule kusoma kutokana na kufahamu kuwa hiyo ni haki yao ya msingi kupata elimu.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Jomu, George Masele alisema kutokana na mwamko walioanza kupata jamii kuhusu kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu wananchi hao wameamua kujenga vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja kwenye shule ya msingi Jomu kwa ajili ya kusoma walemavu.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Tinde B ,Gerald Makiya vinapojengwa vyumba hivyo vya madarasa alisema mradi wa PETS unaofadhiliwa na The Foundition for Civil Society (FCS)umesaidia sana kutokana na jamii kuwa na mwamko kwa kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu.

Mwenyekiti wa Chama cha wasiona Mkoa wa Shinyanga, Marco Nkajiwa alisema mradi wao wa kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma na fedha zinazotolewa na serikali (PETS) katika shule za msingi zenye watoto mchanganyiko na wenye mahitaji maalumu kuwasaidia kusoma vizuri kuna mafanikio mazuri na wito wake kwa jamii waendelea kuwapeleka shule.