Header Ads Widget

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DK MAGUFULI KUJENGA UWANJA MKUBWA WA MPIRA JIJINI DODOMAMgombea urais kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM  Dk  John Magufuli amesema kuwa iwapo atarejea tena  jambo la kwanza atahakikisha anajenga uwanja mkubwa jijini Dodoma.

"Kutokana na wanachama wa CCM kufurika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ili kufuatilia uzinduzi wa Kampeni yetu wa uchaguzi hii ina nipa hamasa ya kujenga uwanja mkubwa kuliko huu na hii ndio kazi nitakayoanza nayo mkinichagua kuwa Rais. "

Mgombea huyo wa Urais wa CCM na Mwenyekiti wa chama hicho Amesema hayo wakati akifungua kampeni  za chama hicho kitaifa hjijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri.