Header Ads Widget

LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA YAHITIMISHWA, SIMBA QUEENS YAKABIDHIWA KOMBE NA SH MILIONI 15


Wachezaji na viongozi wa timu ya Wanawake ya Simba, Simba Queens wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (Serengeti Lite Women Premium League) leo Agosti 12, 2020 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Na Shinyanga Press Club Blog
LIGI Kuu ya Soka la Wanawake Tanzania Bara (SWPL) msimu wa mwaka 2019/2020 imehitimishwa ramsi leo Agosti 12, 2020 kwa timu ya Simba Queens kutwaa ubingwa huo baada ya kufikisha alama 56 katika michezo 22 ya ligi hiyo, ambao wamekabidhiwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Mbali na kukabidhiwa kombe la ubingwa leo, Simba Queens pia wamekabidhiwa zawadi ya Sh Milioni 15 kama mshindi wa kwanza wa ligi, huku waliokuwa mabingwa wa misimu miwili iliyopita mfululizo, JKT Queens wakikabidhiwa Sh Milioni 10 za mshindi wa Pili kwa kufikisha pointi 52.

Vijana wa Alliance Queens wamekabidhiwa Sh Milioni 5 kwa kushika nafasi ya tatu wakifikisha pointi 50, huku Ruvuma Queens wakiambulia nafasi ya nne na alama zao 48.

Mshambuliaji wa klabu ya JKT Queens, Fatuma Mustapha amekuwa mfungaji bora wa ligi hiyo baada ya kupachika mabao 33 kwenye michezo 22.