Header Ads Widget

ARSENAL YATWAA NGAO YA JAMII UINGEREZA


Nahodha wa timu ya Arsenal, Pierre Emerick Aubamayeng akinyanyua ngao ya jamii na kushangilia na wenzake baada ya kushinda mchezo dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita, Liverpool FC leo kwenye Uwanja wa Wembley nchini humo. 

Na Shinyanga Press Club Blog

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta leo amefanikiwa kushinda kikombe cha pili muda mfupi akiwa kama kocha wa timu hiyo, baada ya msimu uliomalizika kushinda ubingwa wa michuano ya FA nchini Uingereza.

Leo, Arsenal imeshinda kombe la Ngao ya Jamii ambao ni maalum kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Uingereza kwa msimu mpya utakaoanza Septemba 12, mwaka huu.

Arsenal wameibuka washindi baada ya kuinyuka Liverpool kwa mikwaju ya Penalti 5 kwa 4 baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1 kwa 1 ndani ya dakika 90.

Bao la Arsenal lilifungwa na Nahodha, Pierre Aubameyang, huku la Liverpool likiwekwa wavuni na Mjapani Takumi Minamino
Wachezaji wa Timu ya Arsenal wakishangilia ubingwa wa ngao ya jamii walioutwaa leo

Furaha ya wachezaji wa Arsenal baada ya kushinda mchezo huo