Header Ads Widget

WATUMISHI 9 TAKUKURU 'WALIOMKWAZA' JPM WASIMAMISHWA


Mkurugenzi Mkuu wa  TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbung'o


MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung'o amewasimamisha kazi watumishi tisa waliohusika katika ujenzi na usimamizi wa majengo Saba, yaliogharimu zaidi ya Sh Bilioni 1.

Majengo hayo yalizinduliwa na Rais Magufuli jana Jumatano na yamejengwa maeneo ya Chamwino, Mpwapwa, Ngorongoro, Manyoni, Masasi, Namtumbo na Ruangwa huku kila jengo likigharimu milioni 140.

Hatua hii imechukuliwa ikiwa ni siku moja mara baada ya Rais John Magufuli kuonesha masikitiko yake juu ya wasimamizi wa ujenzi wa majengo ya Takukuru akieleza kuwa chini ya kiwango.

Rais Magufuli aliweka wazi kusikitishwa juu ya suala hilo huku akiitaka taasisi hiyo kuchukua hatua juu ya wote waliohusika na usimamizi wa ujenzi wa majengo hayo.