Header Ads Widget

SERIKALI KUTUMIA SH. MILIONI 400 KUJENGA SHULE MPYA YA KUMUENZI HAYATI MKAPA

 
 Na Faruku Ngonyani -Mtwara

Wakati shughuli ya kuuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa ukiendelea uwanja wa Uhuru Jijini Dar e salaam, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 400 kujenga shule mpya na ya kisasa kijijini Lupaso.

Hayo yamethibitishwa na aliyekuwa Diwani wa kata ya Lupaso, Dogras Mkapa ambaye ni mtoto wa Mdogo wa Marehemu ambapo amesema kuwa fedha hizo tayari zimeshatolewa na Serikali na mara baada ya taratibu za mazishi kukamilika na mchakato wa ujenzi wa shule hiyo utaanza rasmi.

Aidha Dogras Mkapa amechukua fursa hiyo kwa kumpongeza Rais Dk. John Magufuli na Serikali yake kwa kutenga fedha hizo ili kuijenga shule hiyo na iwe kumbukumbu kwa Hayati Benjamini Mkapa.

Pia amebainisha kuwa wao kama familia wamepokea kwa masikitiko juu ya kifo cha Rais Benjemini Mkapa kwani kuna miradi mingi aliyotaka kuitekeleza kijijini hapo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati, maji n.k.

“Niishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dk John Magufuli kwa kazi mzuri anazozifanya kwa ajili ya watetezi kwa wanyonge, ninavyozungumza hapa tumeweza kupata fedha Sh Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya kisasa kwa ajili ya kumuenzi Rais wetu Benjamin Mkapa,” amesema.